Nenda kwa yaliyomo

Eliud Kipchoge

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Eliud mwaka 2015.

Eliud Kipchoge (alizaliwa Kapsabet, kaunti ya Nandi, 5 Novemba 1984) ni mkimbiaji wa umbali mrefu wa Kenya. Anahesabiwa pengine kama mkimbiaji bora wa marathoni wa nyakati zote.

Tarehe 25 Septemba 2022 alivunja tena rekodi ya dunia kwa kutumia 2.01'09'' tu badala ya 2:01'39'' aliyotumia tarehe 16 Septemba 2018) katika Marathoni ya Berlin.

Maisha binafsi

[hariri | hariri chanzo]

Yeye ndiye wa mwisho kati ya watoto wanne. Alilelewa na mama tu. Alikimbia maili mbili kila siku kwenda shule. Alihitimu kutoka shule ya sekondari ya Kaptel katika mwaka 1999.

Kipchoge alikutana na mwalimu wake, Patrick Sang, mwaka 2000 wakati alipokuwa na miaka kumi na sita.

Sasa, ana mke na watoto watatu ambao wanaishi mji wa Eldoret na yeye anaishi na anafunza katika mji wa Kaptagat, kilomita thelathini kutoka Eldoret.

Mafanikio

[hariri | hariri chanzo]

Eliud Kipchoge anashindana katika marathoni na alishindana katika mita 500.

Kipchoge alishinda marathoni kumi na mbili kati ya kumi na tatu ambazo ameshiriki.

Pia alikuwa na wakati bora zaidi wa marathoni katika jiji la Vienna katika muda wa saa moja wa dakika hamsini na tisa na sekunde arobaini. Kabla ya hapo, watu walifikiri kwamba hakuna mtu ambaye anaweza kukimbia marathoni chini ya muda wa saa mbili. Ingawa alikimbia marathoni haraka kuliko mtu yeyote, marathoni ya Vienna haikuweka rekodi ya dunia, kwa sababu katika marathoni ya Vienna kuli mwongozaji wa mwendo huko na kuli gari lililo na leza ambayo ilionyesha mahali pazuri pa kukimbia barabarani.

Rekodi ya Mashindano

[hariri | hariri chanzo]

Kimataifa

[hariri | hariri chanzo]
MwakaShindanoPahali pa kushindanaNafasiTukioMaelezo
2002Mbio za Dunia za IAAFDublin, EireNafasi ya tano
Nafasi ya kwanza
Mbio za Vijana
Time ya Vijana
23:39
18 pt
2003Mbio za Dunia za IAAF

Mbio za Dunia za Mabingwa
Lausanne, Uswizi

Paris, Ufaransa
Nafasi ya kwanza
Nafasi ya kwanza
Nafasi ya kwanza
Mbio za Vijana
Timu ya Vijana
5000 m
22:47
15 pt
12:52.79
2004Mbio za Dunia za IAAF

Olimpiki
Brussels, Ubelgiji

Athens, Ugriki
Nafasi ya nne
Nafasi ya pili
Nafasi ya tatu
Mbio Ndefu
Timu
5000 m
36:34
30 pt
13:15.10
2005Mbio za Dunia za IAAF

Mbio za Dunia za Mabingwa
Saint-Etienne, Ufaransa

Helsinki, Ufini
Nafasi ya tano
Nafasi ya pili
Nafasi ya nne
Mbio Ndefu
Timu
5000 m
35:37
35 pt
13:33.04
2006Mbio za Dunia za Mabingwa za ndaniMoscow, UrusiNafasi ya tatu3000 m7:42.58
2007Mbio za Dunia ya MabingwaOsaka, UjapaniNafasi ya pili5000 m13:46.00
2008OlimpikiBeijing, UchinaNafasi ya pili5000 m13:02.80
2009Mbio za Dunia za MabingwaBerlin, UjerumaniNafasi ya tano5000 m13:31.32
2010Michezo za Jumuiya za MadolaNew Delhi, UhindiNafasi ya kwanza5000 m13:31.32
2011Mbio za Dunia za MabingwaDaegu, Korea KusiniNafasi ya saba5000 m13:27.27
2012Mbio za Nusu za Marathoni ya DuniaKavarna, BulgariaNafasi ya sitaNusu Marathoni1:01:52
2016OlimpikiRio de Janeiro, BrazilNafasi ya kwanzaMarathoni2:08:44

Marathoni

[hariri | hariri chanzo]
MashindanoNafasiTimuPahali pa kushindanaTarehe
2013 Marathoni ya HamburgNafasi ya kwanza2:05:30Hamburg21 Aprili 2013
2013 Marathoni ya BerlinNafasi ya pili2:04:05Berlin29 Septemba 2013
2014 Marathoni ya RotterdamNafasi ya kwanza2:05:00Rotterdam13 Aprili 2014
2014 Marathoni ya ChicagoNafasi ya kwanza2:04:11Chicago12 Oktoba 2014
2015 Marathoni ya LondonNafasi ya kwanza2:04:42London26 Aprili 2015
2015 Marathoni ya BerlinNafasi ya kwanza2:04:00Berlin27 Septemba 2015
2016 Marathoni ya LondonNafasi ya kwanza2:03:05London24 Aprili 2016
2016 Olimpiki za KiangaziNafasi ya kwanza2:08:44Rio de Janeiro21 Agosti 2016
2017 Marathoni ya BerlinNafasi ya kwanza2:03:32Berlin24 Septemba 2017
2018 Marathoni ya LondonNafasi ya kwanza2:04:17London22 Aprili 2018
2018 Marathoni ya BerlinNafasi ya kwanza2:01:39Berlin16 Septemba 2018
2019 Marathoni ya LondonNafasi ya kwanza2:02:37London28 Aprili 2019
2019 INEOS Marathoni ya Vienna1:59:40Vienna12 Oktoba 2019

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Eliud Kipchoge kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.