Muhimbili

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (Ing.: Muhimbili University of Health and Allied Sciences (MUHAS) ) ni taasisi kubwa ya afya na elimu ya afya iliyoko Dar es Salaam Tanzania.

Kama Chuo cha Elimu ya Afya ilikuwa mwanzoni sehemu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Tangu 2007 imeandikishwa kama Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili. Ndani ya chuo kuna idara nne na taasisi tano.

Idara nne ni kama zifuatazo:

  • Idara ya utaalamu wa meno
  • Idara ya uganga
  • Idara ya uuguzi
  • Idara ya madawa

Kati ya taasisi kuna taasisi za afya ya umma na uganga wa kimila.

Muhimbili ilianzishwa mwaka 1963 ndani ya hospitali iliyoitwa Princess Margaret Hospital na wanafunzi 10 waliofuata kozi za uganga au upasuaji.

Neno Muhimbili limetokana kwa kizaramo "mibili" likimaanisha kiungo cha mtoto tumboni na mama yake (plasenta) Hospitali ilipoanza wazaramo walisema "hapo ndipo wanawake wanapoenda kuacha mibili yao". Neno Muhimbili likazaliwa nalo ladumu hadi leo.

Kwa leo hii Muhimbili ina shule ya madaktari, wauguzi, mafamasia, waganga wa meno, maafisa afya Mazingira, maafisa mazingira na elimu ya juu ya afya.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Tovuti rasmi