Chris Brown

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Chris Brown
Brown akitumbuiza huko mjini Seattle Jingle Bell Bash 8
Brown akitumbuiza huko mjini Seattle Jingle Bell Bash 8
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Christopher Maurice Brown
Amezaliwa 5 Mei 1989 (1989-05-05) (umri 27)
Asili yake Tappahannock, Virginia,
Marekani
Aina ya muziki Pop, R&B, hip hop, dance
Kazi yake Mwimbaji, mtunzi wa nyimbo, dancer, mwigizaji
Aina ya sauti Tenor[1]
Miaka ya kazi 2005–mpaka sasa
Studio Jive, Zomba, LBW
Tovuti www.chrisbrownworld.com

Christopher Maurice "Chris" Brown (amezaliwa tar. 5 Mei 1989) ni msanii wa rekodi za muziki na mwigizaji kutoka nchini Marekani. Ameanza kutoa rekodi yake ya kwanza mwishoni mwa 2005 yenye jina sawa na lake, yaani, Chris Brown akiwa na umri wa miaka 16. Albamu ina kibao kikali cha "Run It!", ambacho kilifikia nafasi ya juu kwenye Billboard Hot 100, na kumfanya Brown kuwa msanii wa kiume wa kwanza kushika nafasi ya kwanza tangu Montell Jordan kuwa naye kutoa kibao na kushika nafasi ya kwanza kwenye chati.[2] Albamu imeuza nakala zaidi ya milioni mbili kwa Marekani na kutunukiwa platinamu mbili mfululuzo na Recording Industry Association of America (RIAA).[3]

Albamu ya pili ya Brown, Exclusive ilitolewa duniani kote mnamo mwezi wa Novemba 2007. Ilitamba na vibao vyake vikali vilivyopata mafanikio makubwa kabisa; kibao chake cha pili kwa U.S. "Kiss Kiss" akimshirikisha T-Pain na "With You", ambao ulishika nafasi ya pili kwenye chati za Billboard Hot 100.[4][5] Brown ametoa toleo la hali ya juu la albamu lililokwenda kwa jina la The Forever Edition. Kibao cha kwanza kutoka kwenye albamu hiyo ni "Forever", kilitolewa mnamo mwezi wa Mei 2008 na kushika nafasi ya pili kwenye chati za Billboard Hot 100.[6] Exclusive has been certified Platinum by the RIAA.[3]

Licha ya kupata mafanikio makubwa akiwa kama msanii wa kujitegemea, Brown amepata kushirikishwa kwenye vibao vingine vikali kama vile "No Air", aliimba pamoja na Jordin Sparks, "Shortie like Mine" sambamba kabisa na rapa Bow Wow na "Shawty Get Loose" na Lil Mama na T-Pain. Kibao hicho kilishika nafasi ya tatu, namba tisa na kumi kwenye chati za Billboard Hot 100 mfululizo.[7][8][9] Kutokana na utaratibu wake wa kucheza, Brown amefananishwa kujulikana kama wasanii wa R&B kama vile Usher na Michael Jackson, wote hudokezwa kama wao ndiyo wenye athira nzima ya muziki wa Brown.[10] Mnamo 2009, Brown alishtakiwa kwa kosa la kumshambulia mwandani wake - mwimbaji Rihanna, na akapigwa kifungo cha nje cha miaka mitano na miezi sita ya mawasiliano ya kihuduma-kijamii na mpenziwe.

1989–2004: Maisha ya awali na shughuli za mwanzo[hariri | hariri chanzo]

Diskografia[hariri | hariri chanzo]

Filmografia[hariri | hariri chanzo]

Televisheni
Mwaka Jina Uhusika Maelezo
2006 Christmas in Washington Chris Brown television special (Turner Network Television)
2007 The O.C. Will Tutt vipengele vitatu
2008 The Suite Life of Zack and Cody Chris Brown nyota mwalikwa
2011 Tosh.O Chris Brown mwalimu wa densi
Filamu
Mwka Jina Uhusika Maelezo
2007 Stomp the Yard Duron small role/film debut
This Christmas Michael 'Baby' Whitfield uhusika mkuu
2009 Blood Rogues Christopher
2010 Takers Jessie Attica[11] Executive Producer
2012 Think Like A Man

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. Moody, Nekesa Mumbi (2007-11-06). Music Review: Chris Brown CD. Yahoo!. Iliwekwa mnamo 2009-01-17.
 2. Chris Brown - Run It! Chart Track. Accharts. Accessed 14 Agosti 2008.
 3. 3.0 3.1 RIAA - Gold & Platinum. RIAA. Iliwekwa mnamo 2009-01-12.
 4. Reuters (2007-11-02). R&B singer Chris Brown tops U.S. singles chart. Yahoo! 7 Music. Iliwekwa mnamo 2008-08-14.
 5. Chris Brown - With You Chart Track. Accharts. Accessed 14 Agosti 2008.
 6. Chris Brown - Forever Chart Track. Accharts. Accessed 14 Agosti 2008.
 7. Billboard - Updated Album Charts from the most Trusted Music Magazine
 8. Shortie like Mine Chart Track. Accharts. Accessed 16 Agosti 2008.
 9. Lil Mama and Chris Brown - Shawty Get Loose - Music Charts. Accharts. Accessed 16 Agosti 2008.
 10. Billy Johnson, Jr. (2008-05-01). Usher, Has Chris Brown Taken Your Spot?. Yahoo! Music. Iliwekwa mnamo 2008-08-16.
 11. Adler, Shawn (2008-10-02). Chris Brown Dances Around Bullets In Upcoming Film 'Bone Deep'. MTV. MTV Networks. Iliwekwa mnamo 2009-02-10.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]


Musical notes.svg Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Marekani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Chris Brown kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.