Bomas of Kenya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Kijiji cha Waluo kwenye Bomas of Kenya

Bomas of Kenya ni makumbusho na maonyesho ya utamaduni wa makabila ya Kenya yanayoonyesha nyumba na vijiji vya kimila kutoka pande nyingi za nchi.

Kuna makumi ya nyumba zilizopangwa pamoja kufuatana na maeneo asilia kwa mfano Waembu, Wakalenjin, Wakamba, Wakikuyu, Wakisii, Wakuria, Waluhya, Waluo, Wamaasai, Wamijikenda au Wataita.

Getini kuna ukumbi mkubwa mwenye nafasi 3,500 uliojengwa kwa namna ya kufanana na nyumba za kimila na katika ukumbi huu kuna maonyesha ya ngoma za makabila ya Kenya. Maonyesho haya hutembelewa na wazalendo na pia watalii.

Ukumbi mkubwa ulikuwa pia mahali pa mikutano ya pekee. Mkutano wa kutunga katiba mpya ulifanyika hapa baada ya uchaguzi wa rais Mwai Kibaki lakini katiba hii haikukubaliwa baadaye na serikali.