Makumbusho ya reli Nairobi
Makumbusho ya reli Nairobi yako karibu na kituo cha reli katika Nairobi, mji mkuu wa Kenya.
Makumbusho hayo yana maonyesho ya injinitreni na mabehewa ya kihistoria kutoka zamani za shirika ya Reli ya Afrika Mashariki.
Makumbusho yalifunguliwa mwaka 1971 na Shirika la reli na bandari la Afrika Mashariki. Baada ya kusambaratika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki ya kwanza yakaendelea kuendeshwa na Shirika la Reli la Kenya. [2]
Makumbusho hadi leo yameunganishwa na njia za reli kwa hiyo ni rahisi kwa mabehewa kutolewa nje kwa matengenezo katika karakana ya reli yenyewe. Vilevile mabehewa mapya yanaweza kuongezwa kirahisi kama sehemu mpya za maonyesho.
Kuna injinitreni za moshi 3 ambazo ziko tayari kufanya kazi; zinatumiwa kwa safari maalumu kama maonyesho nje ya makumbusho.
Injinitreni zinazoonyeshwa kwenye makumbusho zilitengenezwa nje ya Kenya zikafika mwaka 1940 na kupewa majina kufuatana na wilaya za Kenya na Uganda wakati wa ukoloni.
Kiasili injinitreni 10 za makumbusho yalikuwa na namba 77 - 88, baadaye zikawa EAR 5701 - 5712.
Injinitreni za maonyesho
[hariri | hariri chanzo]Makumbusho huonyesha injinitreni mbalimbali pamoja na:[2][3]
Shirika la reli husika | Namba | Jina | Watengenezaji / Kiwanda | aina | Mpangilio magurudumu | Namba ya EAR&H | Hali[4] |
---|---|---|---|---|---|---|---|
Kenya-Uganda Railway | 327 | Vulcan Foundry | ED1 | 2-6-2T | EAR 1127 | maonyesho tu | |
87 | Karamoja | Beyer-Peacock | EC3 | 4-8-4+4-8-4 | EAR 5711 | maonyesho tu | |
2401 | Vulcan Foundry | EB3 | 4-8-0 | maonyesho tu | |||
2409 | Vulcan Foundry | EB3 | 4-8-0 | inatembea | |||
5505 | Beyer-Peacock | GB | 4-8-2+2-8-4 | maonyesho tu | |||
393 | Nasmyth Wilson | EE | 2-6-4T | EAR 1003 | maonyesho tu[5] | ||
Tanganyika Railway | 301 | Beyer Peacock | DL | 4-8-0 | EAR 2301 | maonyesho tu | |
East African Railways | 2921 | Masai of Kenya | North British | Tribal | 2-8-2 | maonyesho tu | |
3020 | Nyaturu | North British | Tribal | 2-8-4 | inatembea | ||
3123 | Bavuma | Vulcan Foundry | Tribal | 2-8-4 | maonyesho tu | ||
5918 | Mount Gelai | Beyer-Peacock | Mountain | 4-8-2+2-8-4 | inatembea | ||
5930 | Mount Shengena | Beyer-Peacock | Mountain | 4-8-2+2-8-4 | maonyesho tu | ||
6006 | Sir Harold MacMichael | Société Franco-Belge | Governor | 4-8-2+2-8-4 | maonyesho tu | ||
Magadi Soda Company | Hugh F Marriott | W.G. Bagnall | 0-4-0ST | maonyesho tu |
Injinitreni Hugh F Marriott ilitengenezwa na kampuni ya W.G. Bagnall mwaka 1951 katika mji wa Stafford nchini Uingereza ikafanya kazi kwa Magadi Soda Company hadi 1970.[6]
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Bomas of Kenya
- Gedi
- Jumba la Mtwana
- Makumbusho ya Garissa
- Makumbusho ya Kabarnet
- Makumbusho ya Kapenguria
- Makumbusho ya Kitale
- Makumbusho ya Narok
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Graeme, Wall. "Kenya- Uganda Railway". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-06-14. Iliwekwa mnamo 28 Februari 2012.
- ↑ 2.0 2.1 Wall, Graeme (30 Oktoba 2009). "Nairobi Railway Museum". Greywall. Greywall Productions. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-01-26. Iliwekwa mnamo 13 Februari 2010.
- ↑ Wall, Graeme (30 Oktoba 2009). "Named Locomotives of East African Railways". Greywall. Greywall Productions. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-07-17. Iliwekwa mnamo 13 Februari 2010.
- ↑ "Locomotives in Kenya". SteamLocomotive. Sunshine Software. 2010. Iliwekwa mnamo 13 Februari 2010.
- ↑ Currently plinthed in Jamhuri Park, Nairobi
- ↑ "Laying the First Rail in Mombasa, May 30, 1896". Worldview 2009. Iliwekwa mnamo 13 Februari 2010.
Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Makumbusho ya reli Nairobi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |