Kangi Alphaxard Lugola
Mhe. Alphaxard Kangi Lugola (Mbunge) | |
Muda wa Utawala 1 Julai 2018 – 23 Januari 2020 | |
Rais | John Magufuli |
---|---|
mtangulizi | Mwigulu Nchemba |
Naibu Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Mamakamu wa Rais Muungano na Mazingira | |
Muda wa Utawala 9 Oktoba 2017 – 1 Julai 2018 | |
Aliingia ofisini Novemba 2015 | |
tarehe ya kuzaliwa | 23 Mei 1963 |
utaifa | Mtanzania |
chama | CCM |
makazi | Dodoma |
mhitimu wa | Chuo Kikuu cha Dar es Salaam |
Kangi Alphaxard Lugola (alizaliwa 25 Mei 1963) ni mwanasiasa Mtanzania na mwanachama wa chama cha kisiasa cha CCM. Amechaguliwa kuwa mbunge wa Jimbo la Mwibara (Mkoa wa Mara) kwa miaka 2015 – 2020 [1].[2]
Alikuwa waziri wa mambo ya ndani kuanzia 1 Julai 2018 hadi kufukuzwa kazi tarehe 23 Januari 2020.
Elimu
Kangi alianza masomo ya shule ya msingi katika shule ya msingi ya Nyabitwebili kuanzia mwaka 1974 mpaka 1977 akasoma pale kuanzia darasa la kwanza hadi la nne na kisha akahamia Shule ya Msingi Mugeta ambapo alisoma pale kwa mwaka mmoja (1978), alipofunga Shule kwa mwaka uliofuata aliamua kwenda kumalizi madara ya sita na saba katika shule ya Msingi Kafunjo, huo ulikuwa mwaka 1979 hadi 1980 hapo ndipo alipohitimu Elimu ya Darasa la saba na hivyo kutunukiwa cheti cha Elimu ya Msingi. Mwaka 1981 alijiunga na Shule ya sekondari ya Sengerema (Sengerema Secondary School) hadi mwaka 1984 alipohitimu Elimu ya sekondari na kutunukiwa cheti cha CSEE. Huo ndio ukawa mwanzo wa kusonga mbele kwani mnamo mwaka 1985 alijiunga tena na Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Songea (Songea Boys Secondary School) kwa ajili ya elimu ya juu ya Sekondari na hivyo kuhitimu kidato cha sita mwaka 1987 kwa kuzawadiwa cheti cha ACSEE. Matokeo hayo yalimpa nafasi Kangi kusonga mbele kwa ajili ya elimu ya juu ambapo mwaka 1996 hadi 1997 alifanikiwa kupata stashada kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam. (University of Dar es Salaam) Kati ya mwaka 1988 hadi mwaka 1992 ambapo alihitimu Shahada ya Uchumi. Mwaka 2008 ajiunga na Chuo kikuu cha Leisester nchini uingereza na kufanikiwa kupata Shahada ya udhamili mwaka 2010.
Ajira
Kangi Lugola alikuwa mwajiriwa wa jeshi la Polisi Tanzania na kuanzia mwaka 1993 hadi mwaka 1998 alikuwa afisa mkaguzi wa Polisi (Inspector) na Mwendesha mashitaka wa serikali, Mwaka 1998 mpaka 1999 alikuwa kaimu afisa mpelelezi mwandamizi wa Jeshi la Polisi, mwaka 1999 hadi 2000 alikuwa mkuu wa kituo daraja la kwanza. Mnamo mwaka 2001 hadi 2002 alikuwa mkuu wa ulinzi na usalama wa uwanja wa ndege na baadaye alihamishiwa katika jumuiya ya afrika mashariki na hapo akapandishwa cheo na kuwa mkuu wa usalama.[3]
Hoja na Misimamo
Kangi Alphaxard Lugola anakumbukwa kwa misimamo yake akiwa bungeni, ama hakika kwa mtu aliyekuwa akifuatilia shughuli za Bunge wakati akiwa katika jumba hilo la kutunga sheria kwa kuwawakilisha wananchi wake. Kangi alikuwa na uwezo mkubwa wa kushawisha na hata ikiwezekana alitumia hata mbinu ya kuchekesha ili mradi hoja yake iungwe mkono. katika mwendelezo wa shughuli za bunge kuna wakati alidhani kwamba akiongea hivihivi huku mtu akimwona akitoa hoja yake atamwonea huruma, ikamlazimu kumwomba idhini spika wa bunge amruhusu avaae kifunikauso ali mradi tu asimuonee huruma waziri mtoa hoja na hiyo ilikuwa katika kuomba maji katika jimbo lake. Kitendo hicho kilimlazimu Spika wa bunge ama akubali ama akatae kutoa idhini, kwa hiyo watu wote hata wapiga kura wa jimbo lake walitamani kusikia Spika akisema chochote, na kwa kawaida ya wapiga kura wao waliliona lile ni jambo zuri kwao kwani ilikuwa ni kiasi gani amwandae waziri kusema chochote kuhusu jimbo lake. Kangi alisema, "Mheshimiwa mimi naomba uniruhusu ni kininja ili nitoe niliyo nayo kwa sababu bila kufanya hivyo nitamuonea huruma Waziri".[4][5]
Jingine ambalo pengine Watanzania wafutiliaji wa masuala ya bunge ambao wamekosa mara baada ya Kangi Lugola kuteuliwa kuwa Naibu Waziri ilikuwa ni ile misimamo yake ya lugha za kuudhi bungeni hakika hakupendezwa nazo na mara kwa mara alikuwa akisikia tu lugha za kuudhi aliinua mkono na kuomba mwongozo kwa Mheshimiwa spika lengo lake likiwa ni kupata ufafanuzi kwa wabunge ambao hupenda kutoa lugha za kuudhi bungeni (matusi) [6]
Kufukuzwa kazi
Rais John Magufuli alitangaza tarehe 23 Januari 2020 kwamba amemfukuza kazi Lugola pamoja na Kamishna wa Zimamoto kutokana na mkataba mbovu wenye thamani ya Euro milioni 408 waliosaini na kampuni ya Romania bila idhini ya wizara ya fedha wala bunge[7]. Tangazo hili lilitolewa katika hotuba ya rais kwenye hafla ya kukabidhi nyumba za maafisa wa gereza la Ukonge mbele ya umati mkubwa wa waandishi wa habari wenye kamera za televisheni [8].
Baada ya kuondoka kwake katika uwaziri uchunguzi ulifunguliwa kuhusu mkataba wa Romania. Tarehe 31 Januari 2020 Lugola alihojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mjini Dodoma. Wakati huohuo, makada wa CCM kwenye jimbo la Bungoma walitangaza nia ya kumhoji Lugola, aliye mbunge wa Bungoma, kuhusu msimamo wake. Tena mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali alidai Lugola aliwahi kusema uwongo mbele ya bunge kuhusu mikataba mbalimbali ya idara yake.
Harakati za kisiasa
Mwaka | Cheo | Ngazi |
---|---|---|
2018 - 2020 | Waziri wa mambo ya Ndani | Serikali ya Muungano wa Jamhuri wa Tanzania |
2017 - 2018 | Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na mazingira | Serikali ya Muungano wa Jamhuri wa Tanzania |
2015 - 2020 | Mbunge Jimbo la Mwibara | Bunge la Jamhuri ya Muungno |
2015 - 2018 | Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Bunge ya mambo ya nje/Mbunge | Bunge la Jamhuri ya Muungno |
2013 - 2015 | Mjumbe Kamati ya Kudumu ya Bunge | Bunge la Jamhuri ya Muungno |
2010 - 2015 | Mbunge Jimbo la Mwibara | Bunge la Jamhuri ya Muungno |
2010 - 2013 | Mjumbe wa kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali/Mbubge | Bunge la Jamhuri ya Muungno |
2008 - 2008 | Mwenyekiti CCM (Wazazi) | Ngazi ya Wilaya |
1986 - 1986 | Mwenyekiti | Ngazi ya Tawi |
Marejeo
- ↑ Tovuti ya Bunge la Tanzania, iliangaliwa Mei 2017
- ↑ https://www.jamiiforums.com/threads/wasifu-wa-waziri-mpya-wa-mambo-ya-ndani-kangi-alphaxard-lugola.1452573/
- ↑ https://www.parliament.go.tz/administrations/199
- ↑ https://www.youtube.com/watch?v=8R3K_ujFN0c
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-05-26. Iliwekwa mnamo 2018-06-13.
- ↑ https://www.youtube.com/watch?v=DOdyPcFU5yE
- ↑ Tanzanian president Magufuli sacks home affaits minister
- ↑ Magufuli sacks minister, commissioner general and permanent secretary over fraud Ilihifadhiwa 24 Januari 2020 kwenye Wayback Machine., video kwenye tovuti ya pulselive.co.ke
Makala hiyo kuhusu mwanasiasa wa Tanzania bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |