Mwigulu Nchemba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mwigulu Nchemba

Mwigulu Lameck Nchemba Madelu ni mwanasiasa Mtanzania na mwanachama wa chama cha kisiasa cha CCM ambaye amekuwa waziri wa fedha na mipango tangu 31 Machi 2021.

Alisoma uchumi kwenye Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam alipohitimu shahada ya uzamili kwenye mwaka 2006.

Amechaguliwa kuwa mbunge wa Iramba Magharibi mwaka 2010 akarudishwa bungeni kwa miaka 20152020. [1] Mwaka 2015 alikuwa makamu wa waziri ya fedha.

Baada ya uchaguzi wa 2015 aliteuliwa kuwa waziri wa kilimo, ila mwaka 2016 alibadilishwa kuwa waziri wa mambo ya ndani.

Mwaka 2018 aliondolewa katika nafasi hiyo na rais John Magufuli aliyetaja kasoro katika wizara yake kama vile ulaji rushwa, matumizi mabaya ya fedha na kuongezeka kwa ajali barabarani ilhali mhusika haonekani[2]. Rais alitaja mkataba wa Lugumi ambako polisi ilipata hasara ya Tsh bilioni 30, kashfa ya mkataba kwa vifaa vibovu kwenye idara ya NIDA, uigizaji wa magari na malori 700 kwa polisi, mkataba usio halali kwa sare za polisi. Pamoja na hayo watazamaji wengine waliuliza kama jinsi Nchemba alivyojaribu kutafuta mapatano na kanisa la KKKT baada ya barua ya maaskofu ya Pasaka 2018 ilijenga wasiwasi wa rais dhidi yake [3].

Katika Februari 2019 Nchemba aliumia katika ajali ambako gari lake liligonga pundamilia wawili barabarani[4]

Tarehe 2 Mei 2020 aliteuliwa kuwa waziri wa Sheria na Katiba baada ya kifo cha waziri Augustine Philip Mahiga.[5]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Tovuti ya Bunge la Tanzania, iliangaliwa Mei 2017
  2. Why Nchemba was sacked from Home Affairs docket Archived 15 Julai 2020 at the Wayback Machine., gazeti The Citizen, tar 3.07. 2018, iliangaliwa Mei 2020
  3. Out in the cold, which way Mwigulu?, The Citizen 04.07.2018, iliangaliwa Mei 2020
  4. Tanzania’s former Home Affairs Minister cheats death as car hits donkeys, Citizen tar. 13.02.2019, iliangaliwa Mei 2020
  5. President Magufuli reinstates Mwigulu Nchemba to cabinet, Citizen 02.05.2020