Augustine Philip Mahiga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Augustine Philip Mahiga (28 Agosti 1945 - 1 Mei 2020) alikuwa mwanasiasa Mtanzania na mwanachama wa chama cha siasa cha CCM.

Aliteuliwa kuwa mbunge na Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa miaka 20152020 na kuwa Waziri wa Mambo ya Nje. [1] Tarehe 3 Machi 2019 alihamishwa kwenye Wizara ya Sheria na Katiba kwa kubadilishawa nafasi na Palamagamba Kabudi aliyepelekwa Wizara ya Mambo ya Nje kutoka ile ya Sheria.

Aliwahi kuwakilisha Tanzania akiwa balozi kwenye Umoja wa Mataifa kati ya miaka 2003 hadi 2010. Kati ya 2010 hadi 2013 aikuwa mkuu wa ofisi ya UM kwa Somalia.

Mahiga alikuwa na elimu ya ualimu (BA kutoka UDSM 1970), akaendelea kusoma Kanada alipohitimu shahada ya uzamivu katika mahusiano ya kimataifa kwenye Chuo Kikuu cha Toronto mwaka 1975. Mwaka 1977 aliingia katika utumishi wa serikali akiajiriwa katika ofisi ya rais. Tangu mwaka 1983 alifanya kazi ya balozi wa Tanzania kwenye vituo mbalimbali.

Aliaga dunia tarehe 1 Mei 2020 mjini Dodoma baada ya kuwa mgonjwa kwa muda mfupi. Sababu ya kifo haijatangazwa.[2][3]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Tovuti ya Bunge la Tanzania, iliangaliwa Mei 2017
  2. Tribune, Emea. "Augustine Mahiga Tanzanian Minister Has Died", Emea Tribune, May 1, 2020. Retrieved on 2020-05-01. Archived from the original on 2020-07-04. 
  3. Tanzanian minister Augustine Mahiga dies at 72 (en-US).