Aleksanda wa Bergamo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Aleksanda alivyochorwa na Bernardino Luini, 1525 hivi.

Aleksanda wa Bergamo (alifariki 286/303) alikuwa askari wa jeshi la Roma ya Kale aliyeuawa kwa kukatwa kichwa wakati wa dhuluma ya Dola la Roma dhidi ya Wakristo[1][2].

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 26 Agosti[3].

Kifodini chake[hariri | hariri chanzo]

Kufuatana na mapokeo ya karne za baadaye alikuwa afisa wa kikosi cha Thebe, kilichoongozwa na Morisi, kilijumlisha wanajeshi Waafrika elfu moja kutoka Misri ya kusini na Nubia waliotumwa Ulaya wakati wa Kaisari Maximiano wa Roma. Wengi wao walikuwa Wakristo.

Huko Agaunum, karibu na mto Rhone, katika eneo la Uswisi wa leo, walipewa amri ya kujiandaa kwa mapigano dhidi ya waasi na kabla ya mapigano kutoa sadaka kwa Kaisari aliyeheshimiwa kama mungu mmojawapo. Wakristo hao walikataa kutoa sadaka hiyo. Kaisari alipopata habari hii akakasirika akatoa amri kuua kila askari wa kumi katika kikosi. Wakristo walipoendelea kukataa amri ilirudiwa hatimaye karibu kikosi chote kiliuawa pamoja na kiongozi chake Morisi.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.