Akademia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Akademia ya Athens, jinsi alivyoiwaza mchoraji Raffael miaka 2000 baadaye


Akademia (kutoka neno la Kigiriki Ἀκαδήμεια, ambalo baadaye likawa Ἀκαδημία akademia) ni shule au chuo kinachotoa elimu au taaluma maalumu, k.v. lugha, muziki, michezo au sanaa.

Jina linarejelea taasisi iliyoundwa na Plato kwenye mwaka 385 KK ilikuwa chuo chake cha falsafa mjini Athens iliyokuwepo ndani ya hekalu ya Athena, mungu wa hekima na elimu.

Pia inaweza kuwa kundi la wasomi wenye ujuzi mkubwa katika taaluma fulani, k.v. siasa, uchumi au masuala ya jamii.

Tena inaweza kuwa taasisi rasmi inayohamasisha maendeleo ya fasihi, sayansi n.k.

Nchi nyingi huwa na "Akademia ya Sayansi" ambayo ni shirika za wataalamu au pia taasisi za wataalamu. Zinalenga kujenga na kuimarisha ushirikiano wa wataalamu wa fani mbalimbali, mbali na kazi yao kwenye vyuo vikuu[1]. Akademia ya Sayansi hailengi kufundisha, inalenga kuunganisha wataalamu na tafiti zao.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Hassan, Mohamed (10 March 2015). "Academies of Science as Key Instruments of Science Diplomacy". Science & Diplomacy 4 (1). 
Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Akademia kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.