Nenda kwa yaliyomo

Adelaide wa Vilich

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Adelaide, Abesi wa Vilich, 1718.

Adelaide wa Vilich, O.S.B. (kwa Kijerumani Adelheid; 970 hivi – 5 Februari 1015), binti Megingoz des Brunharingen, mtawala wa Guelders [1], na Gerberga wa Metzgau, wa ukoo wa kaisari Karolo Mkuu [1], alikuwa abesi wa monasteri mbili nchini Ujerumani.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Tarehe 27 Januari 1966 Papa Paulo VI alithibitisha heshima hiyo.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 5 Februari[2].

Kwanza alijiunga na monasteri ya Mt. Ursula, ambayo ilianzishwa na wazazi wake huko Cologne kufuatana na kanuni ya Jeromu.

Mwaka 980 hivi, walianzisha nyingine huko Vilich, mkabala wa Bonn.

Baada ya kifo cha Gerberga, Adelaide aliingiza kanuni kali zaidi, ile ya Benedikto wa Nursia, akadai masista wajifunze Kilatini ili waelewe Misa.

Sifa za utakatifu na karama yake ya uponyaji zilimvutia Heribert wa Cologne, Askofu mkuu wa Cologne, aliyemfanya abesi wa St. Maria im Kapitol, Cologne.

Ndipo alipofariki, lakini kuzikwa alizikwa Vilich, ambapo tangu hapo sikukuu yake iliadhimishwa kwa fahari ikivuta wengi kuhiji.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. A hagiography, Vita Adelheidis, provides some information regarding her family (Monumenta Germaniae Historica, Scriptores XV, 2).
  2. Martyrologium Romanum
  • RANBECK, The Benedictine Calendar (London, 1896);
  • LECHNER, Martyrologium des Benediktiner-Ordens (Augsburg, 1855);
  • STADLER, Heiligen-Lexikon (Augsburg, 1858);
  • MOOSMUELLER, Die Legende, VII, 448.
  • Friedrich Albert Groeteken, Sankt Adelheid von Vilich, Herrin und Magd, Die rheinisch fränkische Volksheilige und ihre Familie, Butzon & Becker, Kevelaer, 1937, 184 Seiten
  • Jakob Schlafke, Leben und Verehrung der Heiligen Adelheid von Vilich, Köln 1968
  • Josef Niesen, Bonner Personenlexikon, Bouvier Verlag, Bonn 2007

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.