Waraka wa pili kwa Wakorintho
Waraka wa pili kwa Wakorintho ni kati ya vitabu 27 vya Agano Jipya katika Biblia ya Kikristo. Ni kati ya barua mbili zilizomo za Mtume Paulo kwa Wakristo mjini Korintho (Ugiriki).
Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.
Mazingira
[hariri | hariri chanzo]Mdo 19:21-20:1 inasimulia Paulo alivyohama Efeso kutokana na matatizo kuzidi, akaelekea Makedonia na Ugiriki.
Toka huko alipata nafasi ya kuhubiri katika Iliriko, yaani kuanzia Albania ya leo kwenda kaskazini (Rom 15:19).
Wakati huo alipata habari mbaya kuhusu Wakorintho, akawaandikia tena na tena kabla hajawaendea kwa mara ya tatu.
Mpangilio
[hariri | hariri chanzo]Labda kwa kuwa ni mshono wa barua hizo mbalimbali, mpangilio wa 2Kor haueleweki, ingawa ina salamu na shukrani mwanzoni, na salamu nyingine mwishoni kama kawaida.
Katikati mada kuu ni tatu: kujitetea, mchango na mashambulizi dhidi ya wapinzani.
Barua hiyo inatusaidia hasa kumjua Paulo mwenyewe (2Kor 11:1-12:13).
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Tafsiri ya Kiswahili
[hariri | hariri chanzo]- [1] Agano Jipya kwa lugha ya Kiswahili
Vingine
[hariri | hariri chanzo]Wikisource has original text related to this article: |
- "Corinthians, Epistles to the". Encyclopædia Britannica. 7 (11th ed.). 1911. pp. 150–154.
Online translations of Second Epistle to the Corinthians:
- Online Bible at GospelHall.org
- Commentary articles by J. P. Meyer on Second Corinthians, by chapter: 1–2 Archived 15 Juni 2009 at the Wayback Machine., 3 Archived 16 Juni 2009 at the Wayback Machine., 4:1–6:10 Archived 16 Juni 2009 at the Wayback Machine.,
- 6:11–7:16 Archived 16 Juni 2009 at the Wayback Machine.,
- 8–9 Archived 16 Juni 2009 at the Wayback Machine., 10–13 Archived 16 Juni 2009 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mambo ya Agano Jipya bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Waraka wa pili kwa Wakorintho kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |