Tabora (mji)
| Tabora | |
| Mahali pa mji wa Tabora katika Tanzania | |
| Anwani ya kijiografia: 5°0′36″S 32°49′12″E / 5.01°S 32.82°E | |
| Nchi | Tanzania |
|---|---|
| Mkoa | Tabora |
| Wilaya | Tabora |
| Idadi ya wakazi | |
| - Mji | 188,808 |
Tabora ni mji wa kihistoria ya Tanzania ya kati na makao makuu ya mkoa wa Tabora. Eneo lake ni manisipaa na pia wilaya. Mwaka 2002 palikuwa na wakazi 188,808.[1]
Historia [hariri]
Mji ulianzishwa katika nusu ya kwanza ya karne ya 19 na wafanyabiashara Waarabu na Waswahili kutoka Zanzibar. Waliitumia kama kituo kwenye njia ya biashara kati ya pwani na Ziwa Tanganyika. Biashara kuu ilikuwa ndovu pamoja na watumwa. Tabora walijenga nyumba imara pamoja na ghala za bidhaa kwa ajili ya biashara hii. Familia ya Tippu Tip ilikuwa kati ya wenye nyumba wa Tabora.
Mwaka 1871 jeshi la rugaruga wa Mtemi Mirambo ilishambulia mji. Ukajengwa upya. Tangu 1890 Wajerumani walianza kufika na baada ya kushinda Wanyamwezi walifanya Tabora kuwa kitovu chao katika Afrika ya Mashariki ya Kijerumani ya kati; mji ukawa kituo cha kikosi cha jeshi na pia kikosi cha polisi.
Umuhimu wa Tabora ikaongezeka kwa ujenzi wa reli ya kati iliyounganisha pwani na Ziwa Tanganyika ikipita Tabora na karahana muhimu ya reli ikawekwa hapa mjini.
1916 Tabora ilivamiwa na Wabelgiji waliowafukuza Wajerumani lakini baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia mji ukawa sehemu ya Tanganyika.
Usafiri [hariri]
Hadi leo Tabora ni kitovu muhimu cha mawasiliano cha Tanzania ya kati lakini barabara zote zinazofikia mji ni za udongo. Hata hivyo malori kutoka Daressalaam kuelekea Rwanda, Burundi au Kongo hupitia Tabora. Reli inapeleka abiria na mizigo kutoka Tabora kwenda Daressalaam, Kigoma na pia kwenda Mwanza kwa kutumia mkono wa kaskazini ya njia ya reli iliyojengwa wakati wa ukoloni wa Kiingereza.
Kuna pia uwanja mdogo wa ndege.
Marejeo [hariri]
- Red dots are rail lines
- Columbia Encyclopedia, Sixth Edition (at encyclopedia.com)
- Tabora page at fizzylogic.com
| Kata za Wilaya ya Tabora - Mkoa wa Tabora - Tanzania | ||
|---|---|---|
|
Chemchem | Cheyo | Gongoni | Ipuli | Isevya | Itetemia | Itonjanda | Kakola | Kalunde | Kanyenye | Kiloleni | Kitete | Malolo (Tabora) | Mbugani | Misha | Mtendeni | Ndevelwa | Ng'ambo | Tambukareli | Tumbi | Uyui |
||