Mbawahariri

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Zygophlebius)
Mbawahariri
Zygophlebius leoninus
Zygophlebius leoninus
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Neuroptera (Wadudu walio na mabawa wenye vena nyingi kama kimia)
Nusuoda: Myrmeleontiformia (Wadudu kama vitukutuku)
Familia: Psychopsidae (Wadudu walio na mnasaba na mbawahariri)
Handlirsch, 1906
Ngazi za chini

Nusufamilia 2, jenasi 5:

Mbawahariri ni wadudu wadogo kiasi wa familia Psychopsidae katika familia ya juu Myrmeleontoidea wa oda Neuroptera walio na mabawa mapana yafananayo hariri yenye nywele laini nyingi. Kwa hivyo, wanafanana na nondo wadogo. Lava wanafanana na vitukutuku, lakini hawachimbi marima. Badala yake, kwa kawaida huishi kwenye mashina na matawi ya miti, ambapo hulala oteani na kukamata wadudu wengine.

Maelezo[hariri | hariri chanzo]

Mpevu[hariri | hariri chanzo]

Urefu wa mwili ni mm 10-22 na mabawa ya mbele mm 10-35. Kichwa ni kidogo kiasi chenye macho makubwa na vipapasio vifupi. Mabawa ni mapana sana na yana ruwaza ya kushangaza ya vena na madoa.

Lava[hariri | hariri chanzo]

Lava wanafanana na vitukutuku, lakini wamerefuka zaidi na mandibulo hazina meno. Labriamu ni ndefu. Hawana mkundu, labda kwa sababu chakula chao ni kiowevu[1].

Badala ya kuchimba marima (mashimo ya umbo la mpare) huishi kwenye miti ambapo huvizia wadudu wengine na lava wao. Mbuawa anaweza kuwa mkubwa kuliko lava wa mbawahariri.

Spishi za Afrika[hariri | hariri chanzo]

  • Cabralis gloriosus (Msumbiji, Zimbabwe)
  • Cabralis pallidus (Afrika Kusini)
  • Cabralis zambeziensis (JKK, Zambia)
  • Silveira jordani (Namibia, Afrika Kusini)
  • Silveira marshalli (Malawi, Afrika Kusini, Zambia, Zimbabwe)
  • Silveira occultus (Angola, Namibia)
  • Silveira rufus (Afrika Kusini, Zimbabwe)
  • Zygophlebius leoninus (Angola, JKK, Malawi, Msumbiji, Afrika Kusini, Tanzania, Uganda, Zambia, Zimbabwe)
  • Zygophlebius pseudosilveira (Afrika Kusini)
  • Zygophlebius zebra (Kenya, Tanzania)


Picha[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Haug, Gideon T. et al. (2020) The decline of silky lacewings and morphological diversity of long-nosed antlion larvae through time. Palaeontologia Electronica 23(2)