Yosefu Mukasa Balikuddembe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Yosefu Mukasa Balikuddembe († Nakivubo, 15 Novemba 1885), ni mfiadini wa kwanza kati ya Wakristo 22 wa Kanisa Katoliki wanaojulikana na kuheshimiwa duniani kote kama Wafiadini wa Uganda.

Hao walikuwa wahudumu wa ikulu ya kabaka wa Buganda Mwanga II (1884 - 1903) ambao waliuawa kati ya tarehe 15 Novemba 1885 na tarehe 27 Januari 1887 kwa sababu ya kumwamini Yesu Kristo baada ya kuhubiriwa Injili na Wamisionari wa Afrika walioandaliwa na kardinali Charles Lavigerie.

Ndio wafiadini wa kwanza wa kusini kwa Sahara kuheshimiwa na Kanisa Katoliki kama watakatifu.

Mtu wa ukoo Kayozi, alikuwa wa kwanza kuuawa akiwa na miaka 25.