Yosafat wa Polotsk

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Yosafat Kuntsevych)
Mt. Yosafat akiwa amevaa kama askofu mkuu na ameshika tawi la mtende, ishara ya kifodini.

Yosafat wa Polotsk (1580 hivi – 1623) alikuwa askofu wa Polotsk (leo nchini Belarus).

Ametambuliwa na Kanisa Katoliki kuwa mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake ni tarehe 12 Novemba[1].

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Yosafat Kuntsevych (kwa Kibelarus Язафат Кунцэвіч, Jazafat Kuncevič) alizaliwa Wlodzimierz Wolynski katika mkoa wa Volinia (ulikuwa sehemu ya Lithuania, leo ni ya Ukraina) mwaka 1580 au 1584 katika familia ya Waorthodoksi akaitwa Yohane katika ubatizo.

Baada ya kusoma Vilnius (Lithuania), mwaka 1604 alijiunga na Wakatoliki wa mashariki waliokubali mapatano ya muungano wa Brest yaliyoanzisha Kanisa Katoliki la Kigiriki la Ukraine. Akajiunga na wamonaki wa mtakatifu Basili Mkuu kwa jina la Yosafat.

Alipata upadri, akateuliwa kuwa askofu wa Polotsk. Alijitahidi kutunza urithi wa liturgia ya Kiorthodoksi na pia umoja na Kanisa Katoliki kwa jumla.

Alifanya kazi kubwa sana kutunza urithi huo wa pekee wa kanisa lake hadi mwaka 1623 alipouawa na Waorthodoksi waliopinga umoja huo.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.