Yohane Roberts
Yohane Roberts, O.S.B. (1577 - 10 Desemba 1610) alikuwa mmonaki na padri kutoka Wales aliyeuawa na serikali ya Uingereza iliyokuwa imekataza Ukatoliki nchini.
Papa Paulo VI alimtangaza mtakatifu tarehe 25 Oktoba 1970[1].
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifodini chake[2].
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Mtoto wa Waprotestanti, alipokwenda Ulaya bara kwa masomo (1597), alijiunga na Kanisa Katoliki huko Paris, Ufaransa, halafu na monasteri ya Wabenedikto huko Valladolid, Hispania (1598).
Kisha kuweka nadhiri zake (1600) na kupewa upadrisho (1602) alirudi Uingereza kama mmisionari lakini akafukuzwa baada ya wiki chache (1603).[3]
Mwaka huohuo akarudi tena akahudumia waliopatwa na tauni mjini London.
Mwaka 1604 alikamatwa na kufukuzwa tena, lakini akarudi mara moja.
Mwaka 1605 alifungwa gerezani na bada ya miezi saba akafukuzwa tena (1606).
Safari hiyo alibaki Ufaransa miezi 14 akawa Priori wa kwanza wa abasia ya Mt. Gregori, Douai.
Mwaka 1607 alirudi Uingereza akafungwa tena, ila alifaulu kutoroka miezi michache baadaye (1608) hadi alipokamatwa tena (1609).
Badala ya kuuawa kwa kufanya kazi yake kama padri, balozi wa Ufaransa alimuombea afukuzwe tena nchini.
Baada ya kusafiri karibu mwaka mmoja, alirudi kwa mara ya tano Uingereza akakamatwa mwishoni mwa Misa aliyosoma kwa siri, na baada ya siku chache aliuawa huko Tyburn kwa kunyongwa na kukatwa vipandevipande [4].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Saint John Roberts at Catholic.org
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |