Yohane Macias

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sura yake halisi[1].

Yohane Macias, O.P. (Ribera del Fresno, Extremadura, Hispania, 2 Machi 1585Lima, Peru, 16 Septemba 1645) alikuwa bradha wa Shirika la Wahubiri katika nchi ya Peru, rafiki wa Martin de Porres.

Mwaka 1619 alihamia Amerika Kusini[2][3] na miaka 3 baadaye alijiunga na utawa alipodumu kwa uaminifu hadi kifo chake akisali Rozari na kuwatendea kwa huruma wagonjwa na maskini[4].

Mwaka 1837 alitangazwa mwenye heri na Papa Gregori XVI, halafu mwaka 1975 akatangazwa na Papa Paulo VI kuwa mtakatifu[5].

Sikukuu yake ni tarehe ya kifo chake[6].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.