Wamasoni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Lebo ya Umasoni inahusiana na asili ya chama kati ya wajenzi.
Kuingizwa katika chama cha Wamasoni karne XVIII. Lengo la ibada hiyo ni kuachana na maisha ya awali kwa kuigiza kifo na kuzaliwa upya katika maisha ya wanachama.

Wamasoni (yaani Waashi) ni chama cha siri kinachodai kufuata maadili na kustawisha udugu kati ya watu huru.

Msingi wake ni agano kati ya wanachama kwa ajili ya kushirikiana ili kufikia malengo ya pamoja.

Wamasoni wanatamka rasmi kutokuwa na ubaguzi wowote kati yao na kwa wanaotaka kujiunga nao, kufuatana na taratibu zilizopangwa katika Katiba ya waashi huru ambayo iandikwa na James Anderson mwaka 1723 na inakubaliwa na miundo yote ya Kimasoni duniani ingawa kati yake kuna tofauti kadhaa kadiri ya mazingira.

Asili ya chama hicho haijulikani kwa hakika, hasa kabla ya mwaka 1650. Vilevile siri inayotawala maisha ya chama, hata kati ya ngazi mbalimbali za waliojiunga, inafanya iwe vigumu kuelewa malengo halisi na mbinu zinazotumika kuyafikia duniani kote.

Chama kinafanana na dini yenye madhehebu na ibada, hata kumbi zake zinaitwa mahekalu. Mungu anaitwa kawaida Msanii majengo mkuu wa ulimwengu.

Wakatoliki (na baadhi ya Wakristo wengine) hawaruhusiwi kujiunga na chama hicho.

Icon-religion.png Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wamasoni kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.