Nenda kwa yaliyomo

Tutankhamun

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mask ya mazishi ya Tutankhamun
Kaburi la Tutankhamun katika Bonde la Wafalme

Tutankhamun (pia: Tutankhaten, Tutankhamen) alikuwa farao wa Misri ya Kale. [1] Alitawala tangu alipokuwa na umri wa miaka tisa (1334 KK) hadi alipofariki dunia (1323 KK). Alikuwa farao wa nasaba ya 18 (familia ya kifalme) wakati wa Ufalme Mpya.

Yeye ni mashuhuri kwa sababu kaburi lake ni kaburi pekee kati ya makaburi yote ya kifalme ya Misri ya Kale lililohifadhiwa bila kuporwa mali hadi karne ya 20.

Tutankhamun alikuwa mtoto wa Farao Akhenaten na mmoja wa dada wa Akhenaten, [2] au labda mmoja wa binamu zake, Kiya.

Tutankhamun alitawala kwa miaka 9 na alikufa kijana, akiwa na miaka 19. Alikuwa amemwoa dada yake aliyezaliwa na Ankhesenamun, binti ya Malkia Nefertiti, mama yake wa kambo.

Howard Carter akichungulia jeneza la Tutankhamen

Katika mwaka wa tatu wa ufalme wake, Tutankhamun alirudisha nyuma mabadiliko kadhaa yaliyoanzishwa wakati wa utawala wa baba yake. Alimaliza ibada ya mungu Aten na kurudisha ukuu wa mungu Amun. Ibada za Amun ziliruhusiwa tena na marupurupu ya kimapokeo yalirudishwa kwa ukuhani wake. Mji mkuu ulirudi Thebes na mji wa Akhetaten uliachwa.

Alibadilisha pia jina lake mwenyewe kutoka Tutankh-Aten kuwa Tutank-Amun akiimarisha urejeshwaji wa ibada ya Amun.

Ugonjwa na kifo

[hariri | hariri chanzo]

Uchunguzi wa hivi karibuni wa mwili wake kwa kutumia uchunguzi wa CT na vipimo vya DNA unaonyesha alikuwa na watoto wawili, lakini walikufa wakiwa wadogo sana. Wanasayansi sasa wanaamini alikufa kutokana na mguu uliovunjika, uliofanywa kuwa mgumu zaidi na ugonjwa wa mifupa na malaria. [3] Kabla ya ugunduzi huo kulikuwa na nadharia nyingi juu ya kifo chake cha mapema, pamoja na uuaji. Ni hakika kabisa kwamba aliambukizwa aina kadhaa za malaria, na uwezekano mkubwa kwamba alikuwa na kasoro za maumbile zilizosababishwa na kuzaliana kidugu, ilhali mafarao walikuwa na desturi ya kuoa dada zao. Wazazi wake walikuwa kaka na dada. [4] Sababu ya mwisho ya kifo chake bado haijajulikana.

Nyumba mpya katika Jumba la kumbukumbu la Kairo

[hariri | hariri chanzo]

Mnamo 1922 Howard Carter alikuta kaburi la Tutankhamun. Makaburi yote ya mafarao wa Misri yaliporwa mali tangu zamani. Hapa kwa mara ya kwanza kaburi liligunduliwa na kufunguliwa ambalo lilikuwa katika hali asilia. Uchunguzi wa vitu vilivyokaa ndani yake ulileta utajiri wa habari kuhusu maisha ya Misri ya Kale; vitu vingi kutoka kaburi hilo vinaonyeshwa katika jumba la makumbusho la Misri mjini Kairo.

Mnamo 2014 Jumba hilo lilifungua kumbi nne mpya kwenye Jumba la sanaa la Tutankhamun. [5]

  1. Clayton, Peter A. 2006. Chronicle of the Pharaohs: the reign-by-reign record of the rulers and dynasties of Ancient Egypt. Thames & Hudson. ISBN 978-0-500-28628-9
  2. Hawass, Zahi (2010). "Ancestry and Pathology in King Tutankhamun's Family". 303: 640–641. Iliwekwa mnamo 21 Oktoba 2013. {{cite journal}}: Cite journal requires |journal= (help); Unknown parameter |displayauthors= ignored (|display-authors= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Hasan, Lama (2010). "How King Tut died revealed in new study". ABC World News. ABC. Iliwekwa mnamo Desemba 10, 2012.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. Hawass Z. et al 2010. Ancestry and pathology in King Tutankhamun's family. Supreme Council of Antiquities, Cairo, Egypt. JAMA. 303(7):638-47.
  5. BBC News: Egypt unveils renovated Tutankhamun gallery