Thebes

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Coordinates: 25°43′14″N 32°36′37″E / 25.72056°N 32.61028°E / 25.72056; 32.61028

Hekalu ya Luxor, Thebes - Misri
Hekalu ya Karnak, Thebes - Misri
Hekalu ya Hatshepsut, Thebes - Misri

Thebes (kwa Kigiriki: Θῆβαι, Thēbai) ulikuwa mji katika Misri ya Kale karibu km 800 kusini mwa Bahari ya Mediteranea. Ilianza karibu na mji wa kisasa wa Luxor ikaendelea pia kwenye ukingo wa magharibi wa mto Nile ( 25.7° N 32.645° E ).

Thebai lilikuwa jina la Kigiriki, Wamisri wa Kale waliita Waset , ambayo ilikuwa pia jina la mkoa katika Misri ya juu.

Wakati wa Ufalme wa Kati, Farao Mentuhotep II alifanya Waset - Thebes kuwa mji mkuu wa Misri.

Hapo mahekalu makubwa yalijengwa au kupanuliwa ambayo yanaonekana hadi leo. Hasa mahekalu ya Karnak na Luxor hutembelewa na idadi kubwa ya watalii kutoka dunia yote.

Kwenye ukingo wa magharibi wa Mto Nile, wafalme walianza kujenga makaburi pamoja na mahekalu yao. Sehemu mashuhuri zaidi ni Bonde la Wafalme na hekalu la malkia Hatshepsut.

Thebes - Waset ilirudi kuwa mji mkuu mara kadhaa baada ya Mehutep II. Kuna uwezekano kwamba mnamo mwaka 1500 KK Thebes ilikuwa mji mkubwa zaidi duniani kwa wakati wake, ikiwa na wakazi 75,000[1]. Iliharibika wakati wa uasi dhidi ya mfalme Ptolemaio IX mnamo mwaka 84 KK; wakati wa Dola la Roma kikosi cha jeshi kilikaa katika hekalu la kale la Karnak. Mji wa Luxor ya leo ilikuwa kijiji kilichobaki kando ya hekalu la Luxor.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. [https://web.archive.org/web/20110726164950/http://www.ianmorris.org/docs/social-development.pdf Ian Morris, "Social Development Archived 2011-07-26 at the Wayback Machine"]

Vyanzo[hariri | hariri chanzo]

  • Gauthier, Henri. 1925-1931. Dictionnaire des noms géographiques contenus dans les textes hiéroglyphiques . Juzuu. 3 ya 7 vols. Cairo: Imprimerie de l'Institut français d'archéologie orientale du Caire. (Ilichapishwa tena Osnabrück: Otto Zeller Verlag, 1975). 75, 76.
  • Polz, Daniel C. 2001. "Thebes". Katika The Oxford Encyclopedia ya Misri ya kale, iliyohaririwa na Donald Bruce Redford. Juzuu. 3 ya 3 vols. Oxford, New York, na Cairo: Chuo Kikuu cha Oxford Press na Chuo Kikuu cha Amerika huko Cairo Press. 384-388.
  • Redford, Donald Bruce. 1992. "Thebes". In The Anchor Bible Dictionary, iliyohaririwa na David Noel Freedman. Juzuu. 6 ya 6 vols. New York: Doubleday. 442–443.  (seti ya ujazo 6)
  • Strudwick, Nigel C., & Strudwick, Helen, Thebes huko Misri: Mwongozo wa Makaburi na Mahekalu ya Luxor ya Kale . London: Jumba la Habari la Jumba la kumbukumbu la Briteni, 1999,  ) /  (karatasi)

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya Misri bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Thebes kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.