Bonde la Wafalme

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mahali pa bonde katika Milima ya Theban, magharibi mwa Nile, Oktoba 1988 (Rangi nyeusi ni mto Nile na kanda la mashamba yanayomwagiliwa, mshale mwekundu unaonyesha eneo)

Bonde la Wafalme (kwa Kiarabu: وادي الملوك‎ wadi al-muluk) ni bonde la huko Misri ya Kusini. Kuanzia karne ya 16 KK hadi karne ya 11 KK mafarao na wakubwa wao walizikwa huko katika makaburi yaliyochongwa kwenye miamba.[1] [2]

Bonde hilo liko kwenye ukingo wa magharibi wa Mto Nile likitazama mji wa Luxor na mahekalu yake. [3] Baadhi ya wafalme waliozikwa huko ni:

Bonde hilo ni mojawapo kati ya maeneo maarufu ya akiolojia duniani. Mnamo 1979 limepokewa katika orodha ya Urithi wa Dunia, pamoja na makaburi yote ya eneo la Thebes ya kale (Theban Necropolis) [4] Uchunguzi, uchimbaji na uhifadhi unaendelea bondeni ukiongozwa na mamlaka ya Hifadhi ya Urithi wa Utamaduni ya Misri. Kituo kipya cha watalii kimefunguliwa hivi karibuni.

Bonde la Wafalme likiangaliwa kutoka kaskazini.

Jiolojia na hali ya hewa[hariri | hariri chanzo]

Matabaka ya bonde hilo.

Kuna mvua kidogo ya mwaka mzima katika sehemu hii ya Misri, lakini kuna mafuriko ya nadra ambayo hutokea ghafla katika bonde. Yaliwahi kupeleka tani za matope na mawe ndani ya makaburi yaliyokuwa wazi.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Maspero, Gaston (1913). Manual of Egyptian Archaeology, Sixth English Edition. H. Grevel and Co. p. 182. ISBN 1-4219-4169-4. 
  2. Theban Mapping Project. Theban Mapping Project. Iliwekwa mnamo 2006-12-04.
  3. Siliotti, Alberto (1997). Guide to the Valley of the Kings. Barnes and Noble. p. 13. ISBN 88-8095-496-2. 
  4. Ancient Thebes and its necropolis. UNESCO Work Heritage Sites. Iliwekwa mnamo 2006-12-04.

Kusoma zaidi[hariri | hariri chanzo]