Tungo kishazi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Tungo kishazi ni tungo inayotawaliwa na kitenzi. Kitenzi hicho kinaweza kuwa kinajitosheleza kimaana au kisijitoesheleze kimaana vilevile.

Kile kinachojitosheleza kimaana - basi hutoa taarifa kamili wakati kile ambacho hakijitoshelezi kimaana hakitoi taarifa kamili. Hivyo basi ni lazima kiambatane na kishazi (kitenzi) kingine ndipo taarifa yake ikamilike.

Mfano

(i) Mtoto anacheza mpira (ii) Mtoto anayecheza mpira

Tungo zote mbili, yaani, (i) na (ii) zinatawaliwa na kitenzi.

Tungo namba (i)

Inatawaliwa na kitenzi ambacho kimejitosheleza kimaana - hivyo basi kimetoa taarifa kamili.

Tungo namba (ii)

Ijapokuwa tungo hii imetawaliwa na kitenzi, lakini kitenzi hicho hakijitoshelezi kimaana hivyo basi hakitoi taarifa kamili.

Aina za Vishazi[hariri | hariri chanzo]

Kuna aina kuu mbili za vishazi nazo ni:

Kwa mfano:
Ukuta uliobomoka1 ulisababisha hasara kubwa2 1. Kishazi tegemezi
2. Kishazi huru

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tungo kishazi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.