Tomaso wa Villanova
Mandhari
Tomaso wa Villanova, O.S.A. (awali Tomás García y Martínez; Villanueva de los Infantes, 1488 – Valencia, 8 Septemba 1555) alikuwa mtawa Mwaugustino kutoka Hispania maarufu kama mhubiri na mwandishi.
Hatimaye alikubali kwa utiifu tu kuwa askofu mkuu; hapo, pamoja na maadili mengine ya mchungaji bora, aliwaka upendo mkubwa sana kwa maskini wa jimbo lake akawashughulikia hata kumaliza mali yake yote, asibaki hata na kitanda kidogo cha kukilalia [1].
Papa Aleksanda VII alimtangaza mtakatifu tarehe 1 Novemba 1658.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[2].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Wikimedia Commons ina media kuhusu:
- Life of Thomas of Villanova (Augustinians of the Midwest) Archived 15 Novemba 2012 at the Wayback Machine.
- Hotuba za Mt. Tomaso wa Villanova Archived 16 Machi 2016 at the Wayback Machine. Hotuba zake kwa Kilatini