Stergomena Tax

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Stergomena Tax

Stergomena Lawrence Tax (amezaliwa 6 Julai 1960) ni mtumishi wa umma wa Tanzania ambaye aliwahi kuwa Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). [1] [2]. Kwenye Septemba 2021 aliteuliwa kuwa Waziri wa Ulinzi wa Tanzania akiwa mwanamke wa kwanza kuongoza wizara hiyo.

Tarehe 3 Oktoba 2022, Stergomena Tax aliondoka katika wizara hii akipewa nafasi ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania.[3]

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Tax alisoma shule za msingi kadhaa nchini Tanzania na huko Mwanza kwenye Lake Secondary School ambapo alikuwa akisoma pamoja na John Magufuli. [4]

Mnamo 1991 alipata shahada yake ya kwanza katika biashara kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Akaendelea kusoma siasa na uchumi wa maendeleo kwenye Chuo Kikuu cha Tsukuba huko Japani kati ya 1995 hadi 2002 alipohitimu kwa stashada ya uzamili.

Tax ameolewa na ana watoto wawili[5]

Kazi[hariri | hariri chanzo]

2023

Baada ya kurudi Tanzania, alihudumu kama katibu mkuu katika Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki kutoka 2008 hadi 2013 alipoteuliwa kama Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo katika Kusini mwa Afrika katika Mkutano wa 33 wa Wakuu wa Nchi na Serikali huko Lilongwe, Malawi.

Mnamo Agosti 2021, nafasi yake ilichukuliwa na Elias Mpedi Magosi kama katibu wa SADC. Ijumaa, Septemba 10, 2021 aliteuliwa na rais Samia Suluhu Hassan kuwa mbunge. Tarehe 12 Septemba 2021 aliteuliwa kuwa Waziri wa Ulinzi[6].

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Communique of the 33rd Summit of SADC HOSG". SADC. 18 August 2013. Iliwekwa mnamo 19 August 2013.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  2. Ahmed, Maulid (19 August 2013). "Kikwete ends notable SADC term". Daily News (Tanzania). Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-08-23. Iliwekwa mnamo 19 August 2013.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  3. La présidente tanzanienne remanie son gouvernement et met en garde ses rivaux , tovuti ya Sauti ya Marekani, tar. 03.10-2022
  4. Mjasiri, Jaffar (1 September 2013). "Dr Tax: Tanzanians are sitting on a goldmine". Daily News (Tanzania). Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-09-02. Iliwekwa mnamo 2 September 2013.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  5. Tanzania: Dr Stergomena Tax - Doing Tanzania Very Proud, gazeti la Daily News 29.08.2013
  6. Tanzania appoints woman defence minister Archived 13 Septemba 2021 at the Wayback Machine., gazeti la Daily News 13.09.2021

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]