Sigimundi Gorazdowski

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha halisi ya Mt. Sigimundi.

Sigimundi Gorazdowski (kwa Kipolandi: Zygmunt; Sanok, Podkarpackie, Austria-Hungaria, leo nchini Polandi, 1 Novemba 1845Lwów, leo nchini Ukraina, 1 Januari 1920) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki, mwanzilishi wa shirika la Masista wa Mt. Yosefu.[1][2]

Utotoni Gorazdowski aliugua TB hivi ilimbidi asubiri apone kabisa kabla hajapewa upadirisho.[2]

Baadaye alifanya kazi katika parokia mbalimbali akianzisha kwa huruma kubwa nyumba kwa mayatima, wasichana wenye watoto na wahitaji wengineo. Pia aliandika katekisimu na vitabu vingine vya dini kwa watu wake na kutetea uhai wa wasio na sauti.[3][4][5]

Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri huko Ukraine tarehe 26 Juni 2001. Papa Benedikto XVI alimtangaza mtakatifu tarehe 23 Oktoba 2005 huko Vatikano.[4]

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[6].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Saint Zygmunt Gorazdowski. Saints SQPN (31 December 2016). Retrieved on 4 April 2017.
  2. 2.0 2.1 St. Zygmunt has a Cheap Eating House. The Compass (7 January 2010). Retrieved on 4 April 2017.
  3. Saint of the Month. Spirituality for Today (June 2015). Retrieved on 4 April 2017.
  4. 4.0 4.1 San Sigismund Gorazdowski. Santi e Beati. Retrieved on 4 April 2017.
  5. Martyrologium Romanum
  6. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.