Lviv
Nchi | Ukraini |
Kimo | mita |
Eneo | km2 |
Wakazi | 724,713[1] |
Msongamano wa watu | 3,982 |
Lviv (kwa Kiukraini: Львів) ni makao makuu ya Lviv Oblast nchini Ukraini. Jiji hilo lina wakazi 860,000 [2], ilhali asilimia 88 ya watu wanaoishi huko ni Waukraini asilia, % 8 ni Warusi, na % 1 ni Wapolandi.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Katika historia yake, jiji hilo lilikuwa sehemu ya milki na nchi mbalimbali. Liko mahali ambako tamaduni za Polandi na Ukraini zinakutana. Kwa muda mrefu lilikuwa mji wa Kipolandi kwa jina la "Lvov" wenye wakazi wengi kiasi wa Kiyahudi, ilhali Waukraini waliishi katika maeneo ya vijijini ya mazingira ya mji. Hadi mwaka 1772 ilikuwa sehemu ya milki ya Polandi.
Wakati wa kugawiwa kwa Polandi sehemu hii iliwekwa chini ya utawala wa Austria ulioleta Wajerumani, hasa watumishi wa serikali, kuhamia Lvov. Serikali ya Austria ilitumia jina la Kijerumani "Lemberg".
Mwaka 1918 utawala wa Austria ulikwisha na Lvov ilikuwa tena mji wa Polandi. Wayahudi walikuwa takriban theluthi moja ya wakazi.
Mwaka 1939 Polandi ilishambuliwa na Ujerumani, na Jeshi Jekundu la Umoja wa Kisovyeti iliteka mashariki ya Polandi, pamoja na Lvov.
Mwaka 1941 Ujerumani ilishambulia Umoja wa Kisovyeti na kuteka Lvov hadi 1944. Wajerumani walianza mara moja kukusanya Wayahudi na kuwaua. Wayahudi wachache tu waliishi kuona mwisho wa vita na uhuru mpya.
Mwaka 1944 jeshi la Kisovyeti lilirudi mjini, na tangu mwisho wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia 1945 mji ulikuwa sehemu ya Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kiukraini kwa jina la Kiukraini "Lviv". Hii ilifanya Wapolandi wengi kuondoka mjini na kuhamia Polandi yenyewe.
Tangu kuporomoka kwa Umoja wa Kisovyeti Lviv ni mji wa nchi huru ya Ukraini. Wakazi wengi kabisa ni Waukraini.
Leo hii Lviv ni mji unaovuta watalii wengi ambao wanapenda kutembelea kitovu cha kihistoria cha mji chenye majengo mengi ya zamani za Milki ya Austria ambayo yametengenezwa na kukarabatiwa vizuri.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Чисельність наявного населення України на 1 січня 2019 року (PDF) (kwa Kiukraini). State Statistics Service of Ukraine. 2019. uk. 49. ISBN 978-966-8459-82-5.
- ↑ [1] Ilihifadhiwa 28 Septemba 2007 kwenye Wayback Machine. 2001 estimate. URL accessed on June 20, 2006
![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Lviv kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |