Rosa Hope

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mchoro wa Rosa Hope.

Rosa Somerville Hope (Manchester, Uingereza, 8 Juni 1902 - Kokstad, Afrika Kusini, 7 Mei 1972)[1] alikuwa mchoraji Mwingereza ambaye alitembelea Afrika Kusini mwaka 1935 akaendelea kuishi huko.

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Mama yake alikuwa mwalimu katika shule ya Camberwell School of Art na baba yake aliandikwa kama wakala.

Hope alijiunga na shule kwa mara ya kwanza huko Romiley, lakini baadaye alijiunga katika shule ya Manchester High School for Girls pamoja na pacha wake, Muriel Holinger Hope.

Mnamo mwaka 1918 alianza mafunzo katika shule ya sanaa ya Slade School of Art iliyopo London kwa ufadhili na mwaka 1926 alishinda Prix de Rome iliyoonekana katika Royal Academy. Alisoma chini ya Henry Tonks (1862-1937), Phillip Wilson Steer (1860-1942) na John Wheatley (1892-1955). Kwa kipindi hicho alikuwa akiishi huko 40 Downshire Hill, Hampstead katika nyumba ambayo William Hale White, (mwandishi wa riwaya) aliishi mwaka 1852.

Hope alipokwenda Afrika Kusini mnamo mwaka 1935, mwalimu wake wa zamani alimpatia nafasi ya kufundisha katika shule ya Michaelis School of Fine Art katika Chuo Kikuu cha Cape Town. Mnamo mwaka 1938 alikubali nafasi ya mhadhiri mwandamizi katika sanaa katika Chuo Kikuu cha Natal huko Pietermaritzburg, ambapo alibaki mpaka mwaka 1957. Kuanzia hapo alianza safari za mara kwa mara za uchoraji kwenda Drakensberg na Transkei, mara chache akiwa anasindikizwa na rafiki yake mchoraji Phyllis McCarthy.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

People.svg Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Rosa Hope kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.