Robert Luther

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Karl Theodor Robert Luther (Świdnica, 16 Aprili 1822 - Düsseldorf, 15 Februari 1900) alikuwa mtaalamu wa nyota (mwanaastronomia) kutoka nchini Ujerumani.

Alifanya kazi katika Bilk Observatory huko Düsseldorf, Ujerumani, alitafuta asteroidi na kuzigundua 24 kati ya mwaka 1852 na 1890. Ni mshindi wa tuzo ya Lalande mara saba.

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Medali ya ukumbusho wa wana anga watatu,Robert Luther akiwa miongoni mwao

Robert Luther alizaliwa 16 Aprili 1822 na wazazi wake Luther na Wilhelmine von Ende. Alisoma nyumbani na baada ya hapo katika shule ya secondari ya eneo hilohilo. Mnamo 1841 alihamia chuo cha Breslau ambapo alisoma hadi 1843.

Mnamo 1843 Luther alihamia Berlin kusomea masomo ya unajimu. Alikuwa mwanafunzi wa Johann Franz Encke na akamsaidia katika hesabu zake za astronomia. Mnamo 1850 alikua mchunguzi wa pili katika chuo. Mnamo 1851, Franz Brünnow alimwalika Luther kwenye Düsseldorf-Bilk Observatory kuwa mkurugenzi wa uchunguzi baada ya kustaafu kwake. Luther alimuoa Caroline na walikuwa na mtoto mmoja wa kiume, William. Luther alikufa mnamo 1900 kwa ugonjwa mfupi huko Düsseldorf.

Ugunduzi[hariri | hariri chanzo]

Luther aligundua nyota 24 kati ya mwaka 1852 na 1890.

Ugunduzi wake sasa unajulikana kwa kuwa na sifa zisizo za kawaida: Asteroidi zenye sifa sawa, Antiope 90 na glauke inayozunguka polepole sana.

Aligundua asteroidi 25 zifuatazo:

Heshima na tuzo[hariri | hariri chanzo]

Alitunukiwa tuzo ya Lalande mara saba, mnamo miaka ya 1852, 1853, 1854, 1855, 1859, 1860 na 1861 na Royal Astronomical society. Mnamo 1869, alikabidhiwa medali ya ukumbusho ya unajimu.

Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Robert Luther kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.