Pasifiko wa San Severino

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sanamu ya Mt. Pasifiko huko Lendinara.

Pasifiko Divini wa San Severino, O.F.M. (1 Machi 1653 - 24 Septemba 1721) alikuwa mtawa wa shirika la Ndugu Wadogo (tawi la Wareformati) na padri wa Kanisa Katoliki.

Kesi ya kumtangaza mtakatifu ilianza mwaka 1740; Papa Pius VI alimtangaza mwenye heri tarehe 4 Agosti 1786, na Papa Gregori XVI alimtangaza mtakatifu tarehe 26 Mei 1839.

Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 24 Septemba[1].

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Alizaliwa na Antonio Maria Divini na Mariangela Bruni huko San Severino (wilaya ya Macerata, mkoa wa Marche, nchini Italia).

Wazazi wake walifariki muda mfupi baada ya yeye kupata kipaimara, akiwa na umri wa miaka 3.

Alipatwa na tabu nyingi mpaka Desemba 1670, alipovikwa kanzu ya Kifransisko huko Forano.

Alipata upadrisho tarehe 4 Juni 1678, akawa mwalimu wa falsafa (1680-1683) wa watawa vijana wa shirika lake.

Halafu kwa miaka sita akafanya kazi ya kuhubiri katika maeneo ya kandokando.

Baada ya hapo alivumilia kishujaa mateso mengi, kama vile uwete, upofu na uziwi kwa karibu miaka 29.

Kisha kushindwa na ulemavu huo wote asiendelee na utume wa kuhubiri, alikazania maisha ya sala, akijaliwa na Mungu njozi na uwezo wa kutenda miujiza.

Pamoja na hayo, miaka (1692-1693) alikuwa mhudumu wa konventi ya Mt. Maria delle Grazie huko San Severino, alipokuja kufariki.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.