Orodha ya tarehe za ukoloni Afrika

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Hii orodha ya tarehe za ukoloni Afrika inataja miaka ambazo mataifa ya Afrika yalifanywa makoloni au kuwekwa chini ya mamlaka za Ulaya na kupoteza uhuru wao. Inashughulika tu na nyakati za kisasa, si upanuzi wa Wagiriki wa Kale, Dola la Roma, na makabila ya Kigermanik.

Kanda kadhaa, kama Kongo na Jangwa la Sahara, haikuwa na nchi zilizopangwa. Walakini Mfalme Leopold II wa Ubelgiji aliwanyonya vibaya watu na rasilimali za Kongo.

Jedwali la Nchi, koloni na mwaka wa kuanza ukoloni[1]
Namba Nchi Mkoloni Mwaka
01. Moroko Ufaransa 1912
02. Libya Italia 1911
03. Himaya Fulani Ufaransa na Uingereza 1903
04. Eswatini Uingereza 1902
05. Ushirika wa Ashanti Uingereza 1900
06. Burundi Ujerumani 1899
07. Ufalme wa Benin Uingereza 1897
08. Bunyoro Uingereza 1897
09. Dahomey Ufaransa 1894
10. Rwanda Ujerumani 1894
11. Oubangui-Chari Ufaransa 1894
12. Ijebu Ufaransa 1894
13. Botswana Uingereza 1885
14. Merina Ufaransa 1885
15. Zululand Uingereza 1879
16. Fante Confederacy Uingereza 1874
17. Lesotho Uingereza 1868
18. Komoro Ufaransa 1843
19. Algeria Ufaransa 1830
20. Zanzibar Uturuki 1503
21. Mthwakazi (Zimbabwe ya sasa) Uingereza 1893

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. History Ph. D., History M. A., History and Zoology B. A./B.S. "What Were the Colonial Names of African States?". ThoughtCo (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-07-15.