Orodha ya Makaizari wa Byzantini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Orodha hii inataja makaizari wa Bizanti kuanzia nasaba ya Theodosius hadi mwisho wa Dola la Roma Mashariki mwaka wa 1453.

Nasaba ya akina Theodosius[hariri | hariri chanzo]

Miaka ya Utawala Jina la Kaizari Maelezo
28 Machi, 364 hadi 9 Agosti, 378 Valens Alikufa kwenye mapigano ya Adrianopoli.
19 Januari, 379 hadi 17 Januari, 395 Theodosius I Alipewa mamlaka katika Mashariki kutoka kwa Flavius Gratianus aliyekuwa Kaizari wa Magharibi.
17 Januari, 395 hadi 1 Mei, 408 Arkadius Mwana wa Theodosius I
1 Mei, 408 hadi 28 Julai, 450 Theodosius II Mwana wa Arkadius
450 hadi 2 Januari, 457 Markian Amekuwa Kaizari baada ya kumwoa Pulcheria, dada wa Theodosius II

Nasaba ya Thraki[hariri | hariri chanzo]

Miaka ya Utawala Jina la Kaizari Maelezo
7 Februari, 457 hadi 18 Januari, 474 Leo I Ameteuliwa na jenerali Aspar.
18 Januari, 474 hadi 17 Novemba, 474 Leo II Mjukuu wa Leo I.
17 Novemba, 474 hadi 9 Januari, 475 Zeno Baba yake Leo II.
9 Januari, 475 hadi Agosti 476 Basiliskos Shemeji wa Leo I.
Agosti 476 hadi 9 Aprili, 491 Zeno awamo yake ya pili
11 Aprili, 491 hadi 9 Julai, 518 Anastasios I Ameteuliwa na Ariadne, mjane wa Zeno, na kumwoa baadaye.

Nasaba ya akina Justinian[hariri | hariri chanzo]

Miaka ya Utawala Jina la Kaizari Maelezo
Julai 518 hadi 1 Agosti, 527 Justin I
1 Agosti, 527 hadi 14 Novemba, 565 Justinian I Mpwa na mrithi wa Justin I
14 Novemba, 565 hadi 5 Oktoba, 578 Justin II Mpwa na mrithi wa Justinian I
5 Oktoba, 578 hadi 14 Agosti, 582 Tiberios II Labda ameuawa kwa sumu.
14 Agosti, 582 hadi Novemba 602 Maurikios Alimwoa binti wa Tiberios II

Bila nasaba[hariri | hariri chanzo]

Miaka ya Utawala Jina la Kaizari Maelezo
Novemba 602 hadi Oktoba 610 Phokas

Nasaba ya akina Heraklios[hariri | hariri chanzo]

Miaka ya Utawala Jina la Kaizari Maelezo
5 Oktoba, 610 hadi 11 Februari, 641 Heraklios
Februari 641 hadi 24 Mei, 641 Konstantin III Mwana wa Heraklios; Kaizari-Mshiriki pamoja na Heraklonas
Februari 641 hadi Septemba 641 Heraklonas Mwana wa Heraklios; Kaizari-Mshiriki pamoja na Konstantin III
641 hadi 15 Septemba, 668 Konstans II Mwana wa Konstantin III
Septemba 668 hadi Septemba 685 Konstantin IV Mwana wa Konstans II
Septemba 685 hadi 695 Justinian II Mwana wa Konstantin IV
695 hadi 698 Leontios Mnyang'anyi
698 hadi 705 Tiberios III Mnyang'anyi
705 hadi Desemba 711 Justinian II awamo yake ya pili

Bila nasaba[hariri | hariri chanzo]

Miaka ya Utawala Jina la Kaizari Maelezo
Desemba 711 hadi 3 Juni, 713 Philippikos Bardanes
Juni 713 hadi 715 Anastasios II katibu wa Philippikos
715 hadi 717 Theodosius III

Nasaba ya Isauri[hariri | hariri chanzo]

Miaka ya Utawala Jina la Kaizari Maelezo
717 hadi 18 Juni, 741 Leo III
Juni 741 hadi 741 Konstantin V
741 hadi 743 Artabasdos waziri chini ya Leo III
743 hadi 14 Septemba, 775 Konstantin V awamo yake ya pili
Septemba 775 hadi 8 Septemba, 780 Leo IV mwana wa Konstantin V
Septemba 780 hadi 15 Agosti, 797 Konstantin VI mwana wa Leo IV
15 Agosti, 797 hadi 802 Malkia Irene mamake Konstantin VI

Nasaba ya Nikephoros[hariri | hariri chanzo]

Miaka ya Utawala Jina la Kaizari Maelezo
802 hadi 26 Julai, 811 Nikephoros I
Julai 811 hadi Agosti 811 Staurakios mwana wa Nikephoros I
811 hadi Juni 813 Michael I Rangabe alimwoa binti wa Nikephoros I

Bila nasaba[hariri | hariri chanzo]

Miaka ya Utawala Jina la Kaizari Maelezo
Julai 813 hadi 25 Desemba, 820 Leo V

Nasaba ya Frigia[hariri | hariri chanzo]

Miaka ya Utawala Jina la Kaizari Maelezo
25 Desemba, 820 hadi Oktoba 829 Michael II mke wake alikuwa binti wa Konstantin VI
Oktoba 829 hadi 20 Januari, 842 Theophilos mwana wa Michael II, alikuwa Kaizari-Mshiriki tangu 820
20 Januari, 842 hadi Novemba 855 Malkia Theodora I mke wa Theophilos, alimtawalia mwana wake
Novemba 855 hadi 23 Septemba, 867 Michael III mwana wa Theophilos, alitawala kupitia kwa mamake tangu 842

Nasaba ya Makedonia[hariri | hariri chanzo]

Miaka ya Utawala Jina la Kaizari Maelezo
23 Septemba, 867 hadi 29 Agosti, 886 Basil I alimwoa mjane wa Michael III
29 Agosti, 886 hadi 11 Mei, 912 Leo VI mwana wa Basil I, Kaizari-Mshiriki tangu 870
11 Mei, 912 hadi 6 Juni, 913 Alexander III mwana wa Basil I, Kaizari-Mshiriki tangu 879
6 Juni, 913 hadi 9 Novemba, 959 Konstantin VII mwana wa Leo VI, Kaizari-Mshiriki tangu 911
919 hadi 944 Romanos I baba mkwe wa Konstantin VII aliyemtawalia
959 hadi 15 Machi, 963 Romanos II mwana wa Konstantin VII
3 Julai, 963 hadi Desemba 969 Nikephoros II alimwoa mjane wa Romanos II
Desemba 969 hadi 10 Januari, 976 John I alimwoa dada wa Konstantin VII
Januari 976 hadi 15 Desemba 1025 Basil II mwana wa Romanos II
15 Desemba 1025 hadi 11 Novemba 1028 Konstantin VIII mwana wa Romanos II, Kaizari-Mshiriki tangu 976
11 Novemba 1028 hadi 1050 Malkia Zoe binti wa Konstantin VIII
11 Novemba 1028 hadi 11 Aprili 1034 Romanos III mume wa kwanza wa Zoe
Aprili 1034 hadi 10 Desemba 1041 Michael IV mume wa pili wa Zoe
10 Desemba 1041 hadi Aprili 1042 Michael V Mpwa wa Michael IV
Aprili 1042 hadi Juni 1042 Malkia Theodora II Malkia-Mshiriki na dada yake, Zoe
Juni 1042 hadi 11 Januari 1055 Konstantin IX mume wa tatu wa Zoe
11 Januari 1055 hadi Agosti 1056 Malkia Theodora II awamo yake ya pili

Bila nasaba[hariri | hariri chanzo]

Miaka ya Utawala Jina la Kaizari Maelezo
21 Agosti 1056 hadi 31 Agosti 1057 Michael VI jenerali aliyeteuliwa na Theodora II

Nasaba ya akina Komnenos[hariri | hariri chanzo]

Miaka ya Utawala Jina la Kaizari Maelezo
8 Juni 1057 hadi 25 Desemba 1059 Isaak I alijiuzulu kwa sababu ya ugonjwa

Nasaba ya akina Doukas[hariri | hariri chanzo]

Miaka ya Utawala Jina la Kaizari Maelezo
Desemba 1059 hadi 21 Mei 1067 Konstantin X aliteuliwa na Isaak I
21 Mei 1067 hadi 31 Machi 1078 Michael VII mwana wa Konstantin X
Januari 1068 hadi 24 Oktoba 1071 Romanos IV alimwoa mjane wa Konstatin X; Kaizari-Mshiriki na Michael VII
7 Januari 1078 hadi 4 Aprili 1081 Nikephoros III alimwoa mke wa Michael VII wakati ndoa haijatengwa

Nasaba ya akina Komnenos[hariri | hariri chanzo]

Miaka ya Utawala Jina la Kaizari Maelezo
4 Aprili 1081 hadi 15 Agosti 1118 Alexios I Mpwa wa Isaak I
15 Agosti 1118 hadi 8 Aprili 1143 John II mwana wa Alexios I
8 Aprili 1143 hadi 24 Septemba 1180 Manuel I mwana wa John II
24 Septemba 1180 hadi Novemba 1183 Alexios II mwana wa Manuel I
Septemba 1183 hadi 12 Agosti 1185 Andronikos I mpwa wa John II

Nasaba ya akina Angelos[hariri | hariri chanzo]

Miaka ya Utawala Jina la Kaizari Maelezo
12 Agosti 1185 hadi 8 Aprili 1195 Isaak II
8 Aprili 1195 hadi 1 Agosti 1203 Alexios III kaka wa Isaak II
1 Agosti 1203 hadi Januari 1204 Isaak II awamo yake ya pili; Kaizari-Mshiriki na mwana wake
1 Agosti 1203 hadi Januari 1204 Alexios IV mwana wa Isaak II
Januari 1204 hadi 12 Aprili 1204 Alexios V alimwoa binti wa Alexios III

Nasaba ya akina Laskaris[hariri | hariri chanzo]

Miaka ya Utawala Jina la Kaizari Maelezo
Aprili 1204 hadi 1205 Konstantin Laskaris haikuvishwa taji, kwa hiyo hahesabiwi kama Konstantin XI
1205 hadi Novemba 1222 Theodor I kaka wa Konstantin Laskaris
Novemba 1222 hadi 3 Novemba 1254 John III mwana mkwe wa Theodor I
3 Novemba 1254 hadi Agosti 1258 Theodor II mwana wa John III
Agosti 1258 hadi Agosti 1261 John IV mwana wa Theodor II

Nasaba ya akina Palaiologos[hariri | hariri chanzo]

Miaka ya Utawala Jina la Kaizari Maelezo
1259 hadi 11 Desemba 1282 Michael VIII
11 Desemba 1282 hadi Mei 1328 Andronikos II mwana wa Michael VIII
Mei 1328 hadi 15 Juni 1341 Andronikos III mjukuu wa Andronikos II
15 Juni 1341 hadi Mei 1347 John V mwana wa Andronikos III
Mei 1347 hadi 1354 John VI baba mkwe wa John V
1354 hadi 12 Agosti 1376 John V awamo yake ya pili
12 Agosti 1376 hadi 1379 Andronikos IV mwana wa John V
18 Oktoba 1377 hadi 1379 John VII Kaizari-Mshiriki na Andronikos IV
1379 hadi 1390 John V awamo yake ya tatu
miezi michache 1390 John VII awamo yake ya pili
1390 hadi 16 Februari 1391 John V awamo yake ya nne
16 Februari 1391 hadi 21 Julai 1425 Manuel II mwana wa John V; Kaizari-Mshiriki tangu 1373
1399 hadi 1402 John VII awamo yake ya tatu; alimtawalia Manuel II
21 Julai 1325 hadi 31 Oktoba 1448 John VIII mwana wa Manuel II
Januari 1449 hadi 29 Mei 1453 Konstantin XI mwana wa Manuel II