Nenda kwa yaliyomo

Ngugi wa Thiongo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ngugi wa Thiongo

Ngũgĩ wa Thiong'o (amezaliwa 5 Januari 1938) ni mwandishi Mkenya aliyeandika kwa Kiingereza lakini siku hizi anatumia lugha ya Gikuyu.

Maandishi yake ni pamoja na riwaya, tamthilia, hekaya, insha na uhakiki. Ameanzisha gazeti la lugha ya Gikuyu Mũtiiri.

Tangu mwaka 1982 ameishi nje ya Kenya akifundisha kwenye vyuo vikuu mbalimbali kama Yale, New York na Irvine/California.

Ngugi amezaliwa Kenya katika kijiji cha Kamiriithu karibu na Limuru, wilaya ya Kiambu katika jamii ya Wagikuyu akabatizwa James Ngugi. Alikuwa mtoto wa tano wa mke wa tatu wa baba yake Thiong'o wa Nducu. Baba alikuwa mkulima aliyepotea shamba lake kutokana na Waingereza kuteka na kutwaa Nyanda za Juu za Kenya. James alisoma shule za wamisionari za Kamaandura (Limuru), Karinga (Mangu) na Alliance High School (Kikuyu). Katika miaka ile akawa Mkristo. Wakati alikisoma shule familia yake iliathiriwa na vita ya Maumau ikawa kaka yake aliuawa na mama yake aliteswa.

Baada ya kumaliza Alliance High akasoma Makerere akahitimu kupata digrii ya Kiingereza mwaka 1963. Akafunga ndoa na Nyambura mwaka 1961 akazaa naye watoto sita katika miaka iliyofuata. Mwaka 1962 aliandika tamthilia yake ya kwanza "The Black Hermit". Baada ya digrii alirudi Nairobi alipofanya kazi ya uandishi wa gazeti.

Riwaya za kwanza

[hariri | hariri chanzo]

1964 akachukua nafasi ya masomo huko Chuo Kikuu cha Leeds. Hapo Uingereza alitunga riwaya ya "WEEP NOT, CHILD" (1964) akiwa mwandishi wa kwanza kutoka Afrika ya Mashariki aliyetunga riwaya kwa Kiingereza. Alisimulia hadithi ya kijana Njoroge mwenye ndoto ya kuendeleza elimu yake lakini anakwama kati ya ndoto zake na hali halisi ya maisha ya Kiafrika chini ya ukoloni.

Aliendelea kwa "THE RIVER BETWEEN" (1965) akichora picha ya kijiji kilichopasuliwa kati ya wakristo na wafuasi wa dini ya asili. 1967 alitumia historia ya vita ya Maumau na maarifa ya familia yake kwa ajili ya riwaya ya "A GRAIN OF WHEAT".

Mwaka uleule baada ya kuchukua digrii ya pili alirudi Kenya akifundisha Chuo Kikuu cha Nairobi 1967-1969. Aliondoka kwa sababu alipinga kuingia kwa siasa ya serikali katika mambo ya chuo. Baada ya mwaka moja huko Makerere alipata nafasi ya kufundisha Marekani kwenye Chuo Kikuu cha Evanston (1970-71). Mwaka 2013 akatunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu na Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) nchini Tanzania.

Profesa wa fasihi Nairobi

[hariri | hariri chanzo]

1973 alirudi Nairobi kama Profesa wa Kiingereza na mwenyekiti wa idara ya fasihi. Idara hii ilianzishwa kutokana na upinzani wa Ngugi na wenzake dhidi ya hali ya Kiingereza kuwa nguzo kuu ya elimu katika Afrika. Katika makala 'On the Abolition of the English Department' aliyoandika 1968 pamoja na Taban lo Liyong na Henry Owuor-Anyumba, aliwahi kuuliza "Tukihitaji kutazama historia ya utamaduni mmoja kwa undani kwa ajili ya masomo yetu, kwa nini tusichague utamaduni mmoja wa Kiafrika na kuupa kipaumbele ili tulinganishe tamaduni mbalimbali nao?" Kutokana na msimamo huo aliendelea kutafiti fasihi ya simulizi ya makabila ya Kenya, hasa ya Wagikuyu na fasihi ya Kiswahili.

Katika miaka hii huko Nairobi Ngugi aliamua hawezi kuwa tena mkristo. Mwaka 1976 akabadilisha jina lake kutoka James Ngugi kuwa Ngugi wa Thiong'o.

Fasihi simulizi na gereza

[hariri | hariri chanzo]

Kazi yake ya kifasihi ilimpeleka katika mzozo na serikali. Kuanzia mwaka 1976 Ngugi alishirikiana na wanakijiji Wagikuyu karibu na Limuru kuanzisha maagizo ya tamthilia katika lugha yao. 1976 riwaya yake ya "PETALS OF BLOOD" ilichora picha ya watawala wapya Waafrika jinsi walivyochukua nafasi ya wakoloni wa awali wakidharau na kukandamiza wananchi. Mwaka uleule aliandika tamthilia ya "Ngaahika Ndeenda" (Nitaolewa nitakapopenda). Wakubwa katika serikali walikuwa na wasiwasi wakiogopa mwelekeo wa kimarxist wa Ngugi hasa alipotoka katika Chuo Kikuu na kuingia kati ya wananchi wa kawaida kwa njia ya maigizo yake katika lugha ya Gikuyu. Makamu wa Rais wa Kenya Moi aliamua kumkamata Ngugi kwa misingi ya sheria ya usalama wa kitaifa wakati Rais Jomo Kenyatta mwenyewe tayari alikuwa amedhoofika kutokana na uzee na ugonjwa.

Ngugi alikaa mwaka mmoja katika gereza la Kamiti akaandika riwaya ya kwanza kwa Gikuyu "Caitaani mũtharaba-Inĩ" (Shetani msalabani) akitumia karatasi ya choo. Baada ya kuachichwa huru hakuruhusiwa kurudi kazini kwenye Chuo Kikuu. Mwaka 1982 aliondoka Kenya kwenda London.

Maandishi ya baadaye

[hariri | hariri chanzo]

Ngugi ameendelea kutumia Gikuyu pekee kwa ajili ya riwaya lakini amefundisha na kutunga insha kwa Kiingereza. Kati ya maandiko yaliyofuata ni "Detained" (Daiari ya gerezani - 1981); "Decolonizing the Mind: The Politics of Language in African Literature" (Kuondoa ukoloni rohoni - siasa ya lugha katika fasihi ya Afrika 1986) alimodai waandishi Waafrika watumie lugha zao za kienyeji badala la lugha za Kiulaya; Matigari (1987) alimotumia hadithi ya kiutamaduni wa Gikuyu.

Mwaka 2004 Ngugi alirudi mara ya kwanza Kenya lakini alipata maarifa mabaya akishambuliwa na wahuni na kuibiwa mali mke wake akibakiwa. Shabaha muhmu wa ziara yake ilikuwa kutangaza riwaya yake mpya kwa Gikuyu "Muroogi wa Kigogo".

Kiini cha imani ya Ngugi ni ya kwamba kwa kutumia lugha za kienyeji pekee waandishi waafrika watafikia wanachi wa kawaida na kushinda ukoloni mamboleo rohoni. Tatizo alilo nalo hapo ni ya kwamba lugha za kienyeji zinarudi nyuma haraka katika mazingira ya kisasa hata zikiendelea kuzungumzwa na kusikilizwa kwa redio si lazima zinasomwa pia.

Tuzo na heshima

[hariri | hariri chanzo]

Shahada za heshima

[hariri | hariri chanzo]

Maandishi

[hariri | hariri chanzo]

Vitabu vya hadithi

[hariri | hariri chanzo]

Mkusanyiko wa hadithi fupi

[hariri | hariri chanzo]
  • A Meeting in the Dark (1974)
  • Secret Lives, and Other Stories, (1976, 1992)

Tamthiliya

[hariri | hariri chanzo]
  • The Black Hermit (1963)
  • This Time Tomorrow (three plays, including the title play, "The Rebels", and "The Wound in the Heart") (c. 1970)
  • The Trial of Dedan Kimathi (1976)
  • Ngaahika Ndeenda: Ithaako ria ngerekano (I Will Marry When I Want) (1977, 1982) (with Ngugi wa Mirii)
  • Homecoming: Essays on African and Caribbean Literature, Culture, and Politics (1972)
  • Writers in Politics: Essays (1981) ISBN 978-0-85255-541-5 (UK)
  • Decolonising the Mind: The Politics of Language in African Literature (1986)
  • Moving the Centre: The Struggle for Cultural Freedom (1993)
  • Penpoints, Gunpoints and Dreams: The Performance of Literature and Power in Post-Colonial Africa (The Clarendon Lectures in English Literature 1996), Oxford University Press, 1998.

Kumbukumbu

[hariri | hariri chanzo]
  • Detained: A Writer's Prison Diary (1981)
  • Dreams in a Time of War: a Childhood Memoir (2010)
  • In the House of the Interpreter: A Memoir (2012)
  • Birth of a Dream Weaver: A Memoir of a Writer's Awakening (2016)

Kazi nyingine

[hariri | hariri chanzo]
  • Education for a National Culture (1981)
  • Barrel of a Pen: Resistance to Repression in Neo-Colonial Kenya (1983)
  • Mother, Sing For Me (1986)
  • Writing against Neo-Colonialism (1986)
  • Something Torn and New: An African Renaissance (2009) "Queries over Ngugi's appeal to save African languages, culture", Daily Nation, Lifestyle Magazine, 13 June 2009.

Vitabu vya watoto

[hariri | hariri chanzo]
  • Njamba Nene and the Flying Bus (Njamba Nene na Mbaathi i Mathagu, 1986)
  • Njamba Nene and the Cruel Chief (Njamba Nene na Chibu King'ang'i, 1988)
  • Njamba Nene's Pistol (Bathitoora ya Njamba Nene, 1990)
  1. Rollyson, Carl Edmund; Magill, Frank Northen (Juni 2003). Critical Survey of Drama: Jane Martin – Lennox Robinson. Salem Press. uk. 2466. ISBN 978-1-58765-107-6. Iliwekwa mnamo 25 Novemba 2011.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Some of the Prize Winners". Nonino Distillatori S.p.A. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 6 Mei 2014. Iliwekwa mnamo 6 Mei 2014. {{cite web}}: Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help)
  3. 3.0 3.1 "Ehrendoktorwürde der Universität Bayreuth für Professor Ngũgĩ wa Thiong'o (German)". University of Bayreuth. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 6 Mei 2014. Iliwekwa mnamo 6 Mei 2014. {{cite web}}: Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help)
  4. "Ngugi Wa Thiong’o" Archived 23 Oktoba 2016 at the Wayback Machine. Booker Prize Foundation. Accessed 22 October 2016
  5. Flood, Alison, "James Kelman is UK's hope for Man Booker international prize", The Guardian, 18 March 2009. Accessed 22 October 2016.
  6. John Williams. "National Book Critics Circle Names 2012 Award Finalists", The New York Times, 14 January 2012. Retrieved on 15 January 2013. 
  7. "The Nicolas Guillén Philosophical Literature Prize". Caribbean Philosophical Association. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-05-06. Iliwekwa mnamo 6 Mei 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. "Ngugi Wa Thiongo wins 6th Pak Kyong-ni Literature Award". donga.com. Septemba 21, 2016. Iliwekwa mnamo Septemba 24, 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  9. "43rd graduation" (PDF). University of Dar es Salaam. Novemba 2013. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2014-07-26. Iliwekwa mnamo 21 Novemba 2013.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  10. "Yale awards honorary degrees to eight individuals for their achievements". Yale News. 18 Mei 2017. Iliwekwa mnamo 22 Mei 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ngugi wa Thiongo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.