Kamiti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kamiti ni gereza kubwa lililoko Kenya, njia ya kwenda Kiambu. Hapa wengi waliokataa utawala wa kifua uliokuwa ukiendezwa na rais Moi walifungiwa hapa. Kwa muhtasari tu, Ngugi wa Thiong'o, Koigi wa Wamwere walifungiwa hapa bila ya hatia na kutumikia vifungo hadi walipoachiliwa huru.

Hii ilikuwa njama ya kuwamaliza kimwili, kifikra na kimaisha ili watu wasierevuke na wabaki wakinyanyaswa na wakoloni weusi.

Kwa wakati huu Kamiti imekuwa gereza linalofungiwa watenda mabaya kama wezi wa kimabavu, wauaji na wabakaji. Hata kama watu Kamlesh Pattni aliyeifilisisha Kenya katika miaka ya 1990 wamekuwa wageni wa gereza hili, Ketan Somaia, na mjukuu wa Delamere yaani Cholmondeley wamepitia hapa.

Tofauti iliyoko hawa hatuwezi tukasema waliteswa bali hata kifungo walichopewa hakikulingana na hatia walizoshtakiwa.