Nenda kwa yaliyomo

Uzalendo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mzalendo)
Istiari ya Uzalendo katika Sanamu ya Waliofia Hispania, Madrid, (1840), na mchongaji Francisco Pérez del Valle.

Uzalendo (kwa Kiingereza patriotism[1]) ni hali ya mtu kuipenda, kuithamini na kujitoa kwa ajili ya nchi yake kwa msingi wa kabila, utamaduni, siasa au historia. Inakaribiana sana na utaifa.[2][3][4] Uzalendo ukizidi kiasi cha kulitetea taifa huitwa uzalendo kipofu au uzalendo bubu.

Historia

[hariri | hariri chanzo]
Bango la Marekani lenye mandhari ya kizalendo (1917), iliyotolewa na Usimamizi wa Chakula wa Marekani Vita ya Pili ya Dunia

Kwa ujumla dhana ya uraia wema na kujitolea kwa jamii ya watu imerasimishwa duniani kote katika kipindi cha kihistoria.

Katika Zama za Mwangaza wasomi wa karne ya 18 barani Ulaya, uaminifu kwa serikali ulichukuliwa tofauti na uaminifu kwa Kanisa. Ilidaiwa kuwa viongozi wa dini hawapaswi kuruhusiwa kufundisha katika shule za umma kwani uzalendo wao ni wa mbinguni, kwa maana hiyo hawakuweza kuhamasisha wanafunzi wao kupenda nchi yao. Mmoja wa watetezi wenye ushawishi katika dhana hii kubwa ya uzalendo alikuwa Jean-Jacques Rousseau.

Nukuu ya Voltaire: "Inasikitisha kwamba ili kuwa mzalendo mzuri ni lazima uwe adui wa wanadamu wote." [5]

Waelimishaji wa fikra pia walikosoa kile walichokiona kama uzalendo uliokithiri. Mnamo 1774, Samuel Johnson alichapisha kitabu The Patriot, kukosoa kile kinachodhaniwa kuwa uzalendo wa uongo. Jioni ya Aprili 7, 1775, alitoa kauli maarufu, "Uzalendo ni kimbilio la mwisho la mwovu."[6] James Boswell, ambaye alitoa maoni yake katika Maisha ya Johnson, hatoi muktadha wa nukuu. Inadaiwa kuwa Johnson alikuwa akipinga matumizi mabaya ya istilahi "uzalendo" ya John Stuart na wafuasi wake; Johnson alizungumza mahali pengine akitilia mkazo kile kinachoaminika kuwa uzalendo wa "kweli".[7] Hata hivyo, hakuna ushahidi wa moja kwa moja unaokinzana na kile kinachoaminiwa sana kwamba usemi maarufu wa Johnson ulikuwa wa kupinga uzalendo wenyewe.

Umaksi umekuwa na misimamo kadhaa kuhusu uzalendo. Kwa upande mmoja Karl Marx alisema, "Watu wa kazi hawana nchi" na kwamba, "mamlaka ya juu ya tabaka la wafanyakazi litafanya tofauti za kitaifa kupotea haraka." Mtazamo huohuo unakuzwa na Watrotski kama Alan Woods, ambaye "alipendelea kuwasambaratisha watetezi wote wa mipaka ili kutengeneza jumuiya ya ulimwengu wa kijamaa."

Kwa upande mwingine, Wastalini na Wamao wamekuwa wakiupendelea zaidi uzalendo wa kijamaa kulingana na nadharia ya ujamaa ndani ya nchi moja.[8]

Masuala ya falsafa

[hariri | hariri chanzo]

Uzalendo unaweza kuimarishwa na ufuasi wa Dini rasmi (mashirika ya dini au hata mfumo wa utawala). Ni kinyume cha mgawanyiko wa kanisa na serikali kama ilivyodaiwa na wanazuoni ambao waliona uzalendo na imani kama kani zinazofanana na kukinzana.

Michael Billig na Jean Bethke Elshtain wamedai kuwa tofauti baina ya uzalendo na imani ni ngumu kuitambua na hutegemea kwa kiasi kikubwa mtazamo wa mtu mwenyewe.[9]

Christopher Heath Wellman,[10] profesa wa falsafa katika chuo Kikuu cha Washington huko St. Louis, anaeleza kuwa mtazamo maarufu wa nafasi ya "uzalendo" ni jukumu thabiti kwa watu wanaotoka nchi moja na jukumu dogo tu kwa Wasamaria na wageni.[11]

George Orwell, katika insha yake mashuhuri ya ushawishi Maelezo juu ya Utaifa ametofautisha uzalendo na utaifa:

"Kusema 'uzalendo' namaanisha kujitoa kwa ajili ya mahali fulani na mfumo fulani wa maisha, ambao mtu anaamini kuwa ni bora katika dunia lakini si kushurutisha watu wengine. Uzalendo kwa asili yake ni kujihami, kijieshi na kitamaduni. Utaifa, kwa upande mwingine, hauwezi kutenganishwa na shauku ya mamlaka. Lengo la kudumu kwa kila mtaifa ni kupata nguvu zaidi na ufahari zaidi, si kwa ajili yake mwenyewe bali kwa ajili ya taifa au nyingine kitengo kkingine alichochagua kukiambatanisha na nafsi yake." [12]

Masuala maalumu ya kikanda

[hariri | hariri chanzo]

Katika Umoja wa Ulaya, watu wa fikra kama Jürgen Habermas wamepigania "Uzalendo wa Kiuropa", lakini uzalendo katika Ulaya umekuwa ukielekezwa kwa nchi mahalia na mara nyingi zaidi unaendana na kupinga umoja wa Ulaya.

Tafiti kadhaa zimejaribu kupima uzalendo kwa sababu mbalimbali, kama mradi wa Correlates of War ambao umetoa ulinganifu kati ya hulka ya vita na uzalendo. Matokeo kutoka kwenye tafiti tofauti-tofauti yanategemeana na wakati. Kwa mfano, uzalendo katika Ujerumani kabla ya Vita ya Kwanza ya Dunia ndiyo ya juu, wakati leo hii inaonekana kuwa ya chini karibu na mwisho katika tafiti za uzalendo.

Tangu mwaka 1981, World Values Survey imetathmini maadili na imani za watu.[13]

  1. Neno hilo wazalendo lilirasimishwa kwa mara ya kwanza katika Zama za malkia Elizabeth I, kutokea Kifaransa kutoka Kilatini cha karne ya 6: patriota, na hatimaye kutoka Kigiriki πατριώτης (patriōtēs), likimaanisha 'kutoka nchi ya baba', mzizi ukiwa πατρίς patris likimaanisha 'nchi-baba'. "Henry George Liddell, Robert Scott, A Greek-English Lexicon, πατρι-ώτης". Perseus.tufts.edu. Iliwekwa mnamo 2013-11-03. Nomino dhahania [1] uzalendo inaonekana mapema katika karne ya 18. OED
  2. Harvey Chisick. Historical Dictionary of the Enlightenment. Books.google.com. Iliwekwa mnamo 2013-11-03.
  3. "Nationalism (Stanford Encyclopedia of Philosophy)". Plato.stanford.edu. Iliwekwa mnamo 2013-11-03.
  4. "Patriotism (Stanford Encyclopedia of Philosophy)". Plato.stanford.edu. Iliwekwa mnamo 2013-11-03.
  5. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-03-01. Iliwekwa mnamo 2018-04-26.
  6. Boswell, James (1986), Hibbert, Christopher (mhr.), The Life of Samuel Johnson, New York: Penguin Classics, ISBN 0-14-043116-0
  7. Griffin, Dustin (2005), Patriotism and Poetry in Eighteenth-Century Britain, Cambridge: Cambridge University Press, ISBN 0-521-00959-6
  8. Motyl, Alexander J. (2001). Encyclopedia of Nationalism, Volume II. Academic Press. ISBN 0-12-227230-7. {{cite book}}: Invalid |ref=harv (help)
  9. Billig, Michael. Banal Nationalism. London: Sage Publishers, 1995, pp. 56–58.
  10. Christopher Wellman, Professor of Philosophy at Washington University in St. Louis, and Professorial Research Fellow at Charles Sturt University in the Centre for Applied Philosophy and Public Ethics.
  11. Wellman, Christopher Heath (2014). Liberal Rights and Responsibilities: Essays on Citizenship and Sovereignty. New York: Oxford University Press. ku. 32, 50. ISBN 9780199982189.
  12. Orwell, George Essays, John Carey, Ed., Alfred A. Knopf, New York, 2002
  13. Morse, Adair. "Patriotism in Your Portfolio" (PDF). Journal of Financial Markets. 14 (2). U of C 2008: 411–40. doi:10.1016/j.finmar.2010.10.006. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo Novemba 25, 2011. {{cite journal}}: Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Uzalendo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.