Nenda kwa yaliyomo

Mwese

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Kata ya Mwese
Nchi Tanzania
Mkoa Katavi
Wilaya Tanganyika
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 22,171

Mwese ni kata ya Wilaya ya Tanganyika katika Mkoa wa Katavi, Tanzania.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 22,171 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 7,520 waishio humo[2], wengi wao wakiwa Wachagga kutoka mkoa wa Kilimanjaro waliohamishiwa hapo na Mwalimu Nyerere mwanzoni mwa miaka ya 1970.

Hivyo kata ya Mwese inashabihiana na mkoa wa Kilimanjaro kuanzia kilimo cha migomba na kahawa. Katika kata ya Mwese pia wanatumia vinywaji maarufu vinavyopatikana Kilimanjaro kama vile mbege.

Lakini pia wapo wakazi wa makabila mengine kama vile Waha kutoka mkoa jirani wa Kigoma na watu kutoka nchi jirani za Burundi na Kongo.

Pia kuna kabila la Wabende ambao wanajihusisha na kilimo cha mahindi, mihogo na maharage. Wana shughuli za ufuaji wa vyuma kama vile shoka, visu na shughuli za uwindaji pia.

Wafipa kutoka mkoa wa Rukwa, ambao nao shughuli zao ni kilimo, wanapatikana humo. Wapo wachache wa kabila la Watutsi waliopokea uraia na la Wakikuyu ambao walibakia Tanzania baada ya uhuru. Hatimaye kuna jamii kubwa ya wafugaji wa ngomb'e wa jamii ya Wakitiwi.

Kwenye kata ya Mwese kuna mto unaojulikana kama Mto Mapacha ambao unaaminika kuwa wanaokunywa maji yake basi wakikutana wana uwezekano mkubwa wa kupata watoto pacha.

Kata za Wilaya ya Tanganyika - Mkoa wa Katavi - Tanzania
Hadi 2016 wilaya hii ilijulikana kama Mpanda Vijijini

Bulamata | Ikola | Ilangu | Ipwaga | Isengule | Kabungu | Kapalamsenga | Karema | Kasekese | Katuma | Mishamo | Mnyagala | Mpandandogo | Mwese | Sibwesa | Tongwe

Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Katavi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.