Nenda kwa yaliyomo

Hosni Mubarak

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Muhammad Hosni Mubarak)
Hosni Mubarak

Amekufa 25 Februari 2020
Nchi misri
Kazi yake Alikuwa rais

Muhammad Hosni Said Mubarak (Ar. : محمد حسنى سيد مبارك ) b (4 Mei 1928 - 25 Februari 2020) alikuwa rais wa Misri kuanzia 14 Oktoba 1981 hadi 11 Februari 2011.

Mubarak alikuwa mmoja wa watawala wenye mamlaka na nguvu zaidi kwenye eneo la Mashariki ya kati. Alifuata siasa ya rais mtangulizi Sadat aliyepatana amani na Israel. Utawala wake ulikuwa wa kidikteta.

Mubarak alizaliwa na wakulima katika kijiji cha Kafr-El-Meselha kwenye mkoa wa Monufia ulioko Misri ya kaskazini.

Baada ya shule alijiunga na jeshi la anga la Misri akawa rubani akasomeshwa kwenye vyuo vya kijeshi huko Umoja wa Kisovyeti. Baada ya vita ya siku sita akawa mkuu wa jeshi la anga la Misri.

Mwaka 1975 aliteuliwa na rais wa Misri Anwar as Sadat kuwa makamu wa rais. Sadat aliuawa na Waislamu wenye itikadi kali mwaka 1981, hivyo Mubarak akawa rais mpya. Kuanzia 14 Oktoba 1981 alishika vyeo vya rais wa taifa hadi mwaka 2011.

Kuanzia 25 Januari 2011 wananchi wa Misri walifanya maandamano dhidi ya utawala wake na tarehe 11 Februari Mubarak alijiuzulu na kumkabidhi makamu wake madaraka yote.

Mubarak na familia yake walikaa kwenye rasi ya Sinai lakini tarehe 24 Mei 2011 serikali ilimshtaki Mubarak pamoja na wanawe Gamal na Alaa na aliyekuwa mkuu wa polisi ya kisiri Hussein Kamal al-Din Ibrahim Salem kuwa walihusika na mauaji ya waandamanaji 800 wakati wa maandamano wa 2011, pia ufisadi na wizi wa mali ya dola. Kesi ilifunguliwa tarehe 3 Agosti na Mubarak alipelekwa kotini katika kitanda cha hospitali.

Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Hosni Mubarak kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.