Hosni Mubarak

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Hosni Mubarak

Muhammad Hosni Said Mubarak (Ar. : محمد حسنى سيد مبارك ) ( b* 4 Mei 1928) alikuwa rais wa Misri kuanzia 14 Oktoba 1981 hadi 11 Februari 2011.

Mubarak alizaliwa kama mtoto wa wakulima katika kijiji cha Kafr-El-Meselha kwenye mkoa wa Monufia uliopo Misri ya kaskazini. Baada ya shule alijiunga na jeshi la anga la Misri akawa rubani akasomeshwa kwenye vyuo vya kijeshi huko Umoja wa Kisovyeti. Baada ya vita ya siku sita akawa mkuu wa jeshi la anga la Misri.

Mwaka 1975 aliteuliwa na rais wa Misri Anwar as Sadat kuwa makamu wa rais. Sadat aliuwa mwaka 1981 na Waislamu wakali hivyo Mubarak akawa rais mpya. Kuanzia 14 Oktoba 1981 alishika vyeo vya rais wa taifa hadi mwaka 2011. Kuanzia 25 Januari 2011 wananchi wa Misri alianza kuandamana dhidi ya utawala wake na tarehe 11 Februari Mubarak alijiuzulu na kumkabidhi makamu wake madaraka yote.

Mubaraka na familia yake walikaa kwenye rasi ya Sinai lakini tar 24 Mei 2011 serikali ilimshtaki Mubarak pamoja na wanawe Gamal na Alaa na aliyekuwa mkuu wa polisi ya kisiri Hussein Kamal al-Din Ibrahim Salem kuwa waliwajibika kwenye mauaji ya waandamaji 800 wakati wa maandamano wa 2011, pia ufisadi na wizi wa mali ya dola. Kesi ilifunguliwa tar 3 Agosti na Mubaral alipelekwa kotini katika kitanda ya hospitali.

Mubarak alikuwa mmoja wa watawala wenye mamlaka na nguvu zaidi kwenye eneo la Mashariki ya kati. Alifuata siasa ya rais mtangulizi Sadat aliyepatana amani na Israel. Utawala wake ulikuwa wa kidikteta.