Mkoa wa Kati (Kenya)
| ||
Makao Makuu | Nyeri | |
’‘‘Mji Mkubwa’’’ | Nyeri | |
Eneo - Jumla |
Nafasi ya 5 kati ya mikoa ya Kenya 13,191 km² | |
Wakazi - Jumla (2007) - Msongamano wa watu / km² |
Nafasi ya 4 kati ya mikoa ya Kenya 4,145,000 313 /km² | |
Lugha mkoani | Kikuyu Kiembu Kimeru | |
Mkoa wa Kati (Central Province) ni mkoa wa Kenya unaoenea kati ya Mlima Kenya, Nairobi na Nyahururu. Eneo lake si kubwa lakini kuna msongamano mkubwa wa watu kulingana na mikoa ya jirani kwa sababu ya hali ya hewa na rutba ya ardhi inayolisha watu wengi. Nairobi iko nje ya mkoa.
Hali ya hewa
[hariri | hariri chanzo]Hali ya hewa mkoani ni poa hakuna baridi kali kutokana na kimo cha juu. Kuna mvua nyingi kiasi na majira yake ni kuanzia Machi hadi Mei halafu Oktoba hadi Novemba.
Uchumi
[hariri | hariri chanzo]Mkoa wa Kati ni kitovu cha kilimo cha Kenya. Kuna kahawa nyingi pia mazao mengine. Maziwa na bidhaa kutokana na maziwa kama vile jibini hutengenezwa hasa mkoani. Soko zake ni pamoja na mji mkuu wa Nairobi ulio nje ya mkoa mwenyewe lakini imepakana nayo.
Utawala
[hariri | hariri chanzo]Makao makuuy a mkoa yapo Nyeri. Kuna wilaya saba kama zifuatazo:
Wilaya | Wakazi | Makao makuu |
---|---|---|
Nyandarua | 479,902 | Ol Kalou* |
Nyeri | 661,156 | Nyeri |
Kirinyaga | 457,105 | Kerugoya |
Maragua | 387,969 | Maragua |
Murang'a | 348,304 | Murang'a |
Thika | 645,713 | Thika |
Kiambu | 744,010 | Kiambu |
* makao makuu ya awali: Nyahururu |
Historia
[hariri | hariri chanzo]Wenyeji asilia ni hasa Wagikuyu, Waembu na Wameru wanoitwa pia watu wa G.E.M.A. na kushirikiana historia ya pamoja wakitumia lugha ambazo ni karibu. Wanaaminiwa walifika mkoani katika karne ya 17.
Wakati wa ukoloni Waingereza waliona maeneo ya mkoa kufaa kwa walowezi Wazungu kutokana hali ya hewa. Hivyo sehemu kubwa zilitengwa kwa matumizi yao kwa jina la "White Highlands" (Nyanda za juu za Wazungu). Wenyeji wengi waliondolewa mashambani au walivumuliwa tu bila haki.
Siasa hii ilikuwa sababu hasa ya upinzani ulioanzishwa katika miaka ya 1940 kwa jina la Mau Mau.
Chini ya utawala wa rais Kenyatta mkoa uliona miradi mingi ya maendeleo kama barabara, viwanda na shule. Lakini wakati wa utawala wa Moi miradi mingi pamoja na barabara zilirudi nyuma.
Bonde la Ufa | Kaskazini-Mashariki | Kati | Magharibi | Mashariki | Nairobi | Nyanza | Pwani |