Nenda kwa yaliyomo

Milima ya Ufa Mashariki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mlima Kilimanjaro.

Milima ya Ufa Mashariki au Milima ya Afrika Mashariki ni safu mbili za milima ya eneo la Maziwa makubwa ya Afrika, katika nchi za Kenya, Uganda, Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda na Burundi.

Inaitwa hivyo kutokana na uhusiano wake na Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki kati ta mto Zambezi na Bahari ya Shamu; safu ya magharibi ina: Milima ya Virunga, Milima ya Mitumba na Milima ya Rwenzori, wakati ile ya mashariki ina vilele vya juu zaidi katika bara zima la Afrika: Mlima Kilimanjaro (mita 5,895, sawa na futi 19,340) na Mlima Kenya (mita 5,199, futi 17,058). Kati ya milima mingine kuna Mlima Elgon kati ya Kenya na Uganda. Yote, isipokuwa Ruwenzori ina asili ya volkeno.

Milima hiyo kupanda takriban zaidi ya futi elfu kumi na sita na vilele juu hufunikwa na barafu inagawa milima hiyo ni karibu sana na ikweta.[1]

Katika nchi ya Kenya, kuna Mlima Kenya, Milima ya Aberdare, Mharara wa Mau. Juu ya mpaka wa Kenya na Uganda, kuna Mlima Elgon. Kilimanjaro inaenea juu ya mpaka wa nchi ya Tanzania na nchi ya Kenya. Kaskazini mwa Tanzania, kuna Mlima Meru pia. Milima ya Rwenzori ni katikati ya Ziwa Albert na Ziwa Edward juu ya mpaka wa nchi ya Uganda na nchi ya Kongo. Milima ya Virunga yanaenea juu ya mpaka wa nchi wa Uganda, nchi wa Rwanda, na nchi wa Kongo.

Katika nchi ya Kenya, Mlima Lesatima (Satima) ni kilele cha juu katika Milima ya Aberdale na ni futi elfu kumi na tatu mia moja na ishirini. Mharara wa Mau na Milima ya Aberdare yanapanda kutoka sehemu ya mashariki ya Bonde la Ufa wa Mashariki. Mlima Elgon inaanza takriban futi elfu sita mia mbili. Mlima huu una majabali mengi na takriban maili tano mrefu. Wana vilele vengi, lakini Wagagai, ambao kilele juu wa Mlima Elgon, ni futi elfu kumi n nne mia moja na sabini na nane. Mlima Kenya ni pili mlima wa juu katika Afrika. Mlima huu inaenea takriban maili tisini na tano katika upandaji za futi elfu nane. Vilele pacha katika Mlima Kenya ni wanaitwa Batian na Neilion. Kilimanjaro na mlima wa juu katika Afrika yote. Mlima hupanda mpaka futi elfu kumi na tisa mia tatu na arobaini katika kilele Uhuru

Katikati ya Uganda na Kongo, Milima Rwenzori ni maili themanini. Milima Rwenzori pamoja na Mlima Baker na Mlima Gessi, Mlima Stanley, Mlima Speke, Mlima Emin na Mlima Luigi di Savoia.

Katikati Uganda, Kongo, na Rwanda ni Milima ya Virunga ambayo ni ya volkano pia. Volkano katika sehemu ya Kongo zinaitwa Nyamulagira, Nyiragongo, na Mikeno. Volkano juu ya mpaka wa Congo na Rwanda ni Karisimbi na Visoke. Sabinio, Mgahinga na Muhavura ni juu ya mpaka wa Rwanda and Uganda na yanaitwa Milima Mufumbiro.

Wanyama wa Milima ya Afrika Mashariki

[hariri | hariri chanzo]
Sokwe Mkubwa kwenye Milima Virunga.

Wanyama wengi wanaweza kupatikana katika milima ya Afrika Mashariki. Kwa mfano, tembo, kifaru, nyati, paa, nguruwe, nyani wanaishi katika milima hiyo. Milimu Virunga ina sokwe mkubwa ya mlima na nyani wa dhahabu pia. Juu ya Mlima Rwenzori, kuna sokwe wengi.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. "East African mountains | mountains, East Africa". Encyclopedia Britannica (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-04-15.
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Milima ya Ufa Mashariki kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.