Mdororo Mkuu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha ya maandamano ya mwaka 1931 yaliyofanyika kutokana na watu wengi kukosa kazi wakati wa Mdororo Mkuu.

Mdororo Mkuu ulikuwa kipindi ambacho uchumi wa Marekani na sehemu nyingine za dunia ulikuwa mbaya sana. Ulianza na Kuanguka kwa Soko la Hisa la Marekani 1929. Bei za masoko katika Soko la Hisa la Marekani zilianguka kuanzia tarehe 24 Oktoba hadi 29 Oktoba 1929. Watu wengi sana walipoteza kazi zao. Watu wengi wakawa maskini na kutokuwa na makazi. Hii ilimaliza utajiri wa Roaring Twenties. Ile siku ambayo imesemwa kuwa mwanzo wa Mdororo Mkuu inaitwa "Black Tuesday."

Wakati Mdororo Mkuu umeanza, Herbert Hoover ndiye aliyekuwa rais wa Marekani. Watu walipiga kura kwa ajili ya rais mpya hapo 1932. Jina lake lilikuwa Franklin D. Roosevelt. Roosevelt alivyopata serikali akapata kupitisha sheria mpya na mipango ya kusaidia watu ambao walipata kuumizwa na Mdororo Mkuu. Hiyo mipango ilikuwa inaitwa New Deal.

Mdororo Mkuu ulikuwa mbaya sana, lakini kwa msaada wa kila mmoja, kukawa na afadhali, na kila kitu kikaja kuwa sawa. Kati ya miaka 1939 na 1944 watu wengi wakapata kazi tena kwa sababu ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia, na huo Mdororo Mkuu ukawa unaelekea ukingoni na maisha yakawa kawaida na si kama hapo awali.

Kupungua kwa uzalishaji katika tasnia kwenye kilele cha Mdodoro Mkuu
Nchi Kiasi cha kupungukiwa
Marekani − 46,8 %
Poland − 46,6 %
Kanada − 42,4 %
Ujerumani − 41,8 %
Chekoslovakia − 40,4 %
Uholanzi − 37,4 %
Italia − 33,0 %
Ufaransa − 31,3 %
Ubelgiji − 30,6 %
Argentina − 17,0 %
Denmark − 16,5 %
Ufalme wa Maungano (Uingereza) − 16,2 %
Uswidi − 10,3 %
Japani − 8,5 %
Brazil − 7,0 %
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mdororo Mkuu kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mdororo Mkuu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.