Marselino na Petro

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Sanamu ya Mt. Marcellinus huko Seligenstadt.

Marselino na Petro[1] ni Wakristo wa karne ya 3 waliouawa mwaka 304 kwa ajili ya imani yao mjini Roma.

Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 2 Juni[2].

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Kuhusu maisha yao, hatuna habari nyingi za hakika. Marselino alikuwa padri, na Petro mzinguaji. Wote wawili waliuawa kwa kukatwa kichwa katika dhuluma ya Kaisari Diocletian dhidi ya Wakristo wa Dola la Roma.

Simulizi la kifodini chao la Papa Damas I ndilo chanzo cha kale zaidi juu yao. Damas alidai kwamba alipata habari kutoka kwa muuaji wao ambaye baadaye alijiunga na Kanisa[3][4]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Alban Butler, Kathleen Jones, Paul Burns, Butler's Lives of the Saints (Continuum International Publishing Group, 1997), 14.
  2. Martyrologium Romanum
  3. Amore, Agostino (5 Nov 2008). Santi Marcellino e Pietro. Santi e Beati. Iliwekwa mnamo January 9, 2009.
  4. ? (n.d.). SS. Marcellinus and Peter. Eternal Word Television Network. Iliwekwa mnamo January 9, 2009.

Vyanzo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Christian cross.svg Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.