Marie Curie
Maria Curie (jina kamili: Maria Salomea Skłodowska-Curie; 7 Novemba 1867 – 4 Julai 1934) alikuwa mwanafizikia na mwanakemia Mpolandi na Mfaransa aliyepata Tuzo ya Nobel ya Fizikia mwaka 1903 na Tuzo ya Nobel ya Kemia mwaka 1911. Marie Curie ni binadamu pekee aliyepokea tuzo ya Nobel kwa sayansi mbili tofauti.
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Alizaliwa Poland kama Maria Skłodowska wakati nchi hiyo ilipokuwa chini ya Urusi. Wakati ule hapakuwa na nafasi kwa wanawake kusoma kwenye chuo kikuu nchini, hivyo akahamia Ufaransa mwaka 1891 akajiandikisha katika somo la fizikia akaendelea baadaye kuchukua digrii ya hisabati.
Mwaka 1895 akaolewa na mwanasayansi Mfaransa Pierre Curie. Pamoja naye alifanya utafiti wa unururifu akatambua elementi za poloni na radi.
Baadaye alikuwa profesa wa kike wa kwanza katika chuo kikuu cha Sorbonne mjini Paris.
Alikufa kutokana na kansa ya damu (lukemia) kwa sababu maishani mwake alishika dutu nururifu nyingi bila ya tahadhari wakati hatari za unururifu hazijajulikana.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- 1903 Nobel Prize in Physics Archived 28 Julai 2005 at the Wayback Machine. and 1911 Nobel Prize in Chemistry Archived 10 Agosti 2005 at the Wayback Machine. – Tovuti ya kamati ya Tuzo ya Nobel kwa Kiingereza
- Wasifu wa Curie
- The official web page of Maria Curie Skłodowska University in Lublin, Poland Archived 13 Agosti 2006 at the Wayback Machine. (Kiingereza)
Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Marie Curie kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |