Nenda kwa yaliyomo

Makumbusho ya Livingstone

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Makumbusho ya Livingstone ndiyo makumbusho makubwa zaidi katika nchi ya Zambia.

Yanapatikana katika katika jiji la Livingstone, kusini mwa nchi ya Zambia.

Makumbusho hayo huelezea kazi za sanaa na picha, historia, ala za muziki, upelelezi wa David Livingstone na safari za wamisionari wengine.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Makumbusho ya Livingstone ni makumbusho makubwa na ya kale zaidi katika nchi ya Zambia, kwa kuwa yalianzishwa mwaka 1934 kama jumba la makumbusho la David Livingstone.

Mwaka 1948, kapteni A.W. Whittington alijitolea kuuza mabaki ya kale ya binadamu, lakini makumbusho yalikataa kununua mabaki hayo.[1][2]

Mwaka 1951 jengo lilijengwa katika mtindo wa koloni la Wahispania na kufunguliwa.

Jock Millar, meya wa zamani wa Livingstone, alimuomba Harry Susman wa kampuni ya Susman Brothers kujitolea saa iliyokuwa na pande nne kwa ajili ya makumbusho haya lakini kabla ya saa hiyo kutolewa, Susman aliaga dunia.[3]

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Makumbusho ya Livingstone yanapatikana katikati ya jiji la Livingstone, katika barabara ya Mosi-o-Tunya, umbali wa kilometa 10 kutoka maporomoko ya Victoria, kutoka upande wa Zambia, barabara inapatikana katika njia tatu, kilometa 11 kwa kuvuka mpaka wa maporomoko ya Victoria na kuvuka daraja maarufu la Victoria, njia ya pili ni kilometa 60 kutoka mpaka wa Kazungula nchini na kilometa 40 kutoka katika mji mkuu wa Lusaka. Upande wa Botswana, kwa kufuata mto Kafue ni kuvuka daraja kuelekea Mazabuka.[4]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Man. Royal Anthropological Institute of Great Britain and Ireland. 1968. Iliwekwa mnamo 4 Julai 2011.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Clark, J. Desmond; Don R. Brothwell; Rosemary Powers; Kenneth P. Oakley (1968). "Rhodesian Man: Notes on a New Femur Fragment". 3: 105–111. JSTOR 2799415. {{cite journal}}: Cite journal requires |journal= (help)
  3. name="MacmillanD.)2005">Macmillan, Hugh (2005). An African trading empire: the story of Susman Brothers & Wulfsohn, 1901–2005. I.B.Tauris. uk. 192. ISBN 978-1-85043-853-3. Iliwekwa mnamo 4 Julai 2011.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Livingstone Zambia: Livingstone Museum". Guide to Africa. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-04-17. Iliwekwa mnamo 3 Julai 2011.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Makumbusho ya Livingstone kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.