Majadiliano ya mtumiaji:Ivermac
Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!
Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.
Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na b) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.
Kwa mawili matatu labda tazama:
- Kuhusu ukurasa wako wa mtumiaji na kurasa nyingine
- Ukurasa wa mwongozo
- Jamii:Msaada (makala zilizomo humo zinaweza kusaidia mara nyingi)
- Ukurasa wa jumuia (pamoja na Wikipedia:Wakabidhi, penye majina walio tayari kukusaidia)
- Makala za msingi za Wikipedia
Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.
Ujue miiko:
- usilete kamwe matini wala picha kutoka tovuti za nje.
- usiingize matangazo ya kibiashara (pamoja na kuelekeza kwa kurasa zenye matangazo).
- usimwage kamwe matini kutoka google-translate au programu za kutafsiri.
- usitumie kama vyanzo vya taarifa au tanbihi <ref>Wikipedia (au mradi mwingine wa Wikimedia)</ref>, ila unaweza kutumia vyanzo vyake kwa kuvitaja vyenyewe moja kwa moja.
Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!
Welcome to Kiswahili Wikipedia!
We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:
- do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
- nor copied texts/images from other webs to this site!
- do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.
- do not use as references <ref>Wikipedia (or another project of Wikimedia)</ref>, though you can use their references by writing them themselves.
As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.
How can i make an info box appear in my wikipage?
Ukurasa wangu wa wiki wa "Chuo kikuu cha Strathmore" unapoteapotea na nilikuwa nimeshapata alama ya 2.5 katika shindano hili la google/wikipedia. Mtumiaji Rickinyua ana ukurasa huu pia lakini nina uhakika kuwa mimi ndiye niliyeandika ukurasa huu wa kwanza.Nawaomba tafadhali mtatue shida hii.
Salam. Husika na kichwa cha habari hapo juu. Ni makala ambayo imeanzishwa awali na Ndugu Timothy mnamo tar. 15 Desemba, 2009. Lakini wewe pia umeanzisha makala ileile bila hata kutazama kama makala ipo au la. Kwa tukio hili, unaombwa usiiorodheshe kwenye orodha yako ya submission. Kwa sababu moja kati ya hizi itafutwa. Kila la kheri.--MwanaharakatiLonga 08:37, 22 Desemba 2009 (UTC)
Makala ya Pepe Kalle
[hariri chanzo]Salaam! Ivermac hongera! Umepiga hatua. Sasa hivyo ndiyo makala za Kamusi Elezo zinavyotakiwa kuwa... Basi ni mwanzo mzuri wa kuendeleza wikipedia yetu. Kila la kheri.--MwanaharakatiLonga 10:11, 6 Januari 2010 (UTC)
Shukrani
[hariri chanzo]Nashukuru sana kwa pongezi lako.Hii itanipa motisha zaidi
Makala bila maelezo yoyote
[hariri chanzo]Salaam! Ndugu, unaandika makala bila chochote ndani yake. Mfano: Zablon Amanaka - na kuna nyingine nyingi tu ambazo umeandika hivyo-hivyo. Si vizuri - cause this is litle bit awkward! Samahani sana, ni lazima uache kufanya hivyo. Maana yake ukiendelea kufanya hivyo kila siku itakuwa kama tunakomoana kwa kweli. Jitahidi!--MwanaharakatiLonga 07:07, 20 Januari 2010 (UTC)
My View
[hariri chanzo]How am i then supposed to book the wiki pages for the kiswahili wikipedia competition so that other competitors dont write on the articles that i have booked. We were told to do so when the competitoin started so that is shows that you are the first one who booked that page and that you are working on it.
- Sawa. But so far, nothing has been added on the last pages. You've created a bunch of an empty articles - which is very bad for the project. I strongly advise you that, stop doing it anymore. Cause you will not get anything, though! Also, it's quite unnecessary to book the wiki pages. It's better to write even a short articles, rather than that ones which you've created - it is somewhat pathetic. Cheers.--MwanaharakatiLonga 17:30, 21 Januari 2010 (UTC)
makala zihitajizo habari
[hariri chanzo]Ndugu Ivermac, salaam! Wakati wa shindano, makala nyingi zimeanzishwa bila kuwekewa yaliyomo hata kidogo, nasi wanawikipedia hatukuwa na nafasi ya kurekebisha sana. Kwa hiyo sasa, naomba tusaidiane kusawazisha hizo makala. Kwa mfano, ungeweza kuanza kwa kuangalia orodha ya makala bila jamii. Bila shaka utagundua kadhaa ambazo ni duni, labda yenye maneno mawili matatu tu. Ndivyo nilivyogundua k.m. na makala ya Henri Fayol, mhandisi Mfaransa wa karne ya 19. Sasa ukiangalia mabadiliko niliyoyaingiza utapata mambo ya msingi ya wikipedia. K.m. naingiza kigezo cha {{DEFAULTSORT}} kwa ajili ya orodha ya makala katika jamii ifuate alfabeti vizuri. Tena naingiza jamii za miaka ya kuzaliwa (k.m. [[Jamii:Waliozaliwa 1841]]) na ya kufariki (k.m. [[Jamii:Waliofariki 1925]]). Pia, ikiwa ni makala fupi bila maelezo mengi, naingiza kigezo cha {{mbegu-mtu}} (yaani kama ni mtu). Hatimaye, naingiza kiungo kwa wikipedia ya Kiingereza (k.m. [[en:Henri Fayol]]) ambapo naweza kupata code kwa picha ya mtu (k.m. [[Image:Fonds henri fayol.jpg|thumb|right|Henri Fayol]]) pamoja na habari nyingine. Nitashukuru kwa msaada wako katika kuboresha makala mpya zilizoachwa duni. Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 07:16, 3 Februari 2010 (UTC)
Jibu Langu
[hariri chanzo]Asante sana kuomba usiadizi wangu.Nikipata muda nitajaribu iwezekanavyo kuzirekebisha kurasa hizo kwani mimi huwa na kazi nyingi za darasa.Iwapo nitapata nafasi nitazirekebisha
- Asante sana kwa jibu lako. Unisamehe nikiendelea kuandika kuhusu usafishaji wa wikipedia baada ya shindano. Nimefurahi sana kuona jinsi ilivyokua wikipedia yetu. Sasa lakini, tukiendelea kuboresha makala zilizoongezeka, tuwe makini. Kabla hatujaongeza au kurekebisha habari za makala fulani, lazima tuangalie majadiliano na ukurasa wa historia ya makala hiyo. Angalia k.m. makala ya uchumi. Ukiihariri bila kuangalia majadiliano yake wala historia yake, inawezekana utaongeza kazi ya baadaye kwa vile tafsiri za shindano zilizofuta makala za zamani (pamoja na jamii na interwiki zake) hazijaunganishwa. Nitaendelea kutafuta makala kama hiyo na kuziandikia katika majadiliano yake. Kwa ajili ya kuunganisha tafsiri mbili au zaidi, labda itasaidia ukifungua zote, kila moja katika dirisha lake, na kunakilisha sehemu za makala za zamani kwenda katika makala ya sasa. Pole na kazi. Na asante kwa kazi yako. (Pia, ukiandika kwenye kurasa za majadiliano waweza kutia sahihi na tarehe kwa kutaipu ~~~~ ukiwa umesajiliwa kama Ivermac.) Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 04:14, 4 Februari 2010 (UTC)
Kuondoa yaliyomo ya ukurasa
[hariri chanzo]Bw Ivermac salaam nimeona uliondoa yaliyomo yote katika kurasa tatu (Chuo kikuu cha Kikristu cha Pan-Africa, Nemanja Vidic, Stephen Appiah). Hii haitakiwi. Kwa kawaida ni sababu ya kumsimamisha mwanawikipedia kwa muda fulani. Sichukui hatua hii kwa sababu nafikiri ulikuwa na nia njema. Nakubali makala hizi tatu hazistahili kuwemo. Ukiona makala usiofaa utaratibu ni:
- kama umbo (lugha, muundo yaliyomo) ni baya andika hoja lako kwenye ukurasa wa majadiliano; kama baada ya siku 2 hakuna jibu, endela kama b)
- makala ni makala inayoonekana haifai (haina yaliyomo, lugha isiyoeleweka kabisa, muundo wa fujo, inaonekana imenakiliwa mahali) upendekeza ifutwe. kwa hii chukua hatua ifuatayo:
- hariri ukurasa, andika JUU ya makala {{futa}} na kuhifadhi. Sasa unaona mraba mdogo juu ya makala yenye maandishi
Kuna pendekezo la kufuta makala hii. Ona majadiliano kwenye ukurasa wa majadiliano na hapa.
- Bonyeza kwenye "hapa" utafika ukurasa wa makala yaliyopendekezwa kwa ufutaji. Hapa fungua kwa uhariri, anzisha kifungu kipya ukifuata mifano iliyopo tayari. Jina la makala unayotaka ifutwe weka kama kichwa chenye mabano mraba ===[[Jina la Makala]]===. Chini yake andika sentensi 1 kwa nini unataka ifutwe.
- Baada ya masaa, siku, wakati mwingine wiki mkabidhi ataangalia makala. --Kipala (majadiliano) 10:59, 10 Februari 2010 (UTC)
Samahani
[hariri chanzo]Samahani sana kuondoa habari za kurasa hizo.Sababu yangu ya kuondoa ni kwamba kurasa mbili za Steven Appiah [[1]] na Chuo Kikuu cha Kikristo cha Pan Africa [[2]] nilikwisha ziandika hapo awali lakini katika kurasa tofauti na kurasa nilizozitoa zilikuwa na jina langu niliona hakuna haja ya kuwa na kurasa mbili; moja yenye habari na moja ambayo haina habari. Ukitaka hakikisho angalia ukurasa huu wa wikipedia [[3]] kisha utazame kurasa za mtumiaji Ivermac ambaye ni mimi. Niwie raddi