Nenda kwa yaliyomo

Stephen Appiah

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Steven Appiah)
Stephen Appiah
Senior career*
MiakaTimuApps(Gls)
1995–1997Hearts of Oak21(19)
1997–2000Udinese36(0)
2000–2003Parma29(0)
2002–2003Brescia (loan)31(7)
2003–2005Juventus48(3)
2005–2008Fenerbahçe SK64(11)
2009–Bologna0(0)
Timu ya Taifa ya Kandanda
1996–Ghana56(14)
* Senior club appearances and goals counted for the domestic league only and correct as of 8 Februari 2007.

† Appearances (Goals).

‡ National team caps and goals correct as of 8 Februari 2007
Stephen Appiah

Stephen Appiah (amezaliwa 24 Desemba 1980) alikuwa mwanakandanda wa kimataifa wa kiungo cha kati kutoka Ghana na nahodha wa timu ya taifa ya Ghana.

Wasifu wa Klabu

[hariri | hariri chanzo]

Appiah alianza katika klabu ya mtaa ya Hearts of Oak mwaka 1995, akiwa na umri wa miaka 15. Mwaka wa 1996 alifanyiwa majaribio na klabu ya Galatasaray SK kuchezea kikosi chao cha vijana lakini hakutiwa saini na alirudi kwa klabu yake ya Hearts ya Oak.

Mwaka wa 1999, kiungo huyu wa Uingereza ya Crystal Palace. Alikaa huko kwa muda wa misimu mitatu, na ilikuwa katika uwanja wao(Crystal Palace) wa Selhurst Park ambapo aligeuka kutoka kuwa mshambuliaji hadi kuwa mchezaji wa kiungo mwenye dutu. Appiah alishikilia jukumu la kulinda safu ya ulinzi katika mechi yake ya kwanza dhidi ya Derby.

Mwaka wa 2000, uhamisho wake kwenda klabu ya Parma ulitumbukia nyongo baada ya kuambukizwa na virusi ya hepatitis, lakini Appiah alipona kutoka kwa ugonjwa huu kuihamia Parma katika majira ya joto ya mwaka wa 2000. Mghana huyu alikuwa katika pindo la kuwa mchezaji wa mara kwa mara katika uwanja wa Stadio Ennio Tardini lakini klabu ilidhani itasaidia maendeleo yake iwapo atapeanwa kama mchezaji mkopo kwa klabu ya Brescia kwa msimu wa 2002-03. Kama mchezaji wa mara kwa mara wa Lombardians, Appiah alifunga mara saba katika mechi 31.

Hii iliwahamasisha mabingwa watetezi wa Serie A Juventus kwa talanta zake. Juventus iliilipa Parma jumla ya yuro (€) milioni 2, katika majira ya joto ya mwaka wa 2003, ili kupata huduma za Appiah kama mchezaji wa mkopo na chaguo la uhamaisho wa kudumu wa kitita cha yuro (€) milioni 6 mwaka wa 2004.

Mwaka wa 2003, Stephen Appiah aliteuliwa na kumaliza katika nafasi ya 8 kwa tuzo la mchezaji bora wa mwaka wa bara Afrika. Alienda kufurahia msimu imara wa kwanza katika klabu ya Juventus katika uwanja wa Stadio delle Alpi, kwa kucheza mechi 30 za Serie A, kucheza katika fainali ya Coppa Italia iliyoshindwa na klabu ya Lazio katika mechi zote mbili za marudiano na kucheza mechi yake ya kwanza katika Kombe la Mabingwa barani Ulaya. Ingawa Appiah alipoteza nafasi yake katika timu ya kwanza kwa Manuele Blasi mapema katika msimu wake wa pili, alicheza mechi 18 za Serie A huku Juventus ikiishinda taji la Serie A kwa mara wa 28.

Mnamo Julai 2005, yeye alihamishwa kutoka Juventus kwenda Fenerbahçe SK, mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Uturuki kwa kitita cha yuro (€) milioni 8. Alishinda taji ya ligi kuu ya Uturuki akiwa katika klabu ya Fenerbahçe katika mwaka wa mia moja tangu kuanzishwa kwa klabu. Katika mwisho wa msimu wa 2006-07, Appiah alionyesha hamu ya kuhama kutoka Fenerbahçe ijapokuwa klabu ilitaka kuendeleza mkataba wake wa wakato huo.

Baada ya jeraha la goti lililomweka nje ya mchezo kwa muda mrefu, Appiah aliingia kama mbadala katika mechi ya Fenerbahçe ya ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya PSV Eindhoven tarehe 7 Novemba 2007, kuashiria kupona kwake kamili. Appiah alikwenda nchini Italia na kufaulu katika ukarabati wa jeraha lake. Jeraha hili la muda mrefi lilimlazimu kiungo huyu wa kati kukosa kushiriki katika mchuano wa Kombe la Mataifa ya Afrika la mwaka wa 2008 ambayo Ghana walibanduliwa katika hatua ya nusu fainali. Alifaulu kuachiliwa kwa bure na klabu yake ya Fenerbahçe kutokana na matatizo yake ya kuumia kila mara.

Appiah alienda kujaribiwa na klabu yenye makao mjini London, Tottenham mnamo Januari 2009 akiwa na mtazamo wa kupewa mkataba wa kudumu wa miezi 6, hata hivyo wasiwasi kuhusu goti lake na kiwango chake cha mazoezi kulisababisha kutopewa kwake kwa mkataba, kwani Spurs ilichukua fursa ya kumsaini Wilson Palacios kutoka Wigan Athletic badala yake. Mwezi uliyofuata Appiah alikwenda majaribioni katika klabu ya FC Rubin Kazan, lakini mabingwa hawa wa Urusi waliamua dhidi ya kumsaini mchezaji huyu kwa sababu ya wasiwasi wa kiwango chake cha mazoezi. Licha ya kuwa bila klabu tangu kuondoka kwake kutoka Fenerbahçe mnamo Juni 2008, Appiah alibakia mchezaji wa mara kwa mara na timu ya kitaifa katika msimu wotw wa 2008-09.

Mnamo 1 Novemba 2009 Bologna alitangaza kumaliza kumsaini Appiah kwa uhamisho wa bure.

Juhudi nyinginezo

[hariri | hariri chanzo]

Appiah ana lebo ya nguo, iitwayo StepApp, ambayo itatolewa mwishoni mwa Novemba, katika mji wake wa nyumabni wa Accra huku pesa zote ambazo zitalipwa kwa ajili ya nguo hizi zikipelekwa kwa StepApp Foundation. Lebi hii ya nguo itatolewa kwanza barani Afrika kabla ya kuwasili barani Ulaya na Marekani katika miezi zifuatazo.

Wasifu wa Kimataifa

[hariri | hariri chanzo]

Pamoja na timu ya kitaifa ya Ghana, ameshiriki katika kombe la dunia la vijana wasiozidi umri wa miaka 17 mwaka wa 1995, mashindano ya vijana ya miaka ya 1997 na 1999, shindano la Olimpiki la mwaka mwa 2004 na Kombe la dunia la mwaka wa 2006, ambapo timu hiyo ya kitaifa ilifika katika hatua ya raundi ya pili.

Akiwa Hearts ya Oak
  • Kombe la FA la Ghana:1996
  • Ligi kuu ya Ghana:1997
Akiwa Parma FC
  • Coppa Italia:2001-02
Akiwa Juventus FC
  • Supercoppa Italiana:2003
  • Serie A:2004-2005]
  • Serie A:2005-2006
Akiwa Fenerbahçe SK
  • Ligi kuu ya Uturuki;2006-07
  • Kombe la Super Cup la Kiuturuki:2006-07
Akiwa na timu ya taifa ya Ghana
  • Bingwa katika kombe la dunia la FIFA la vijana wasiozidi umri wa mika 17 mwaka wa 1995

Kibinafsi

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]