Zablon Amanaka
Jinsia | mume |
---|---|
Nchi ya uraia | Kenya |
Tarehe ya kuzaliwa | 1 Januari 1976 |
Mahali alipozaliwa | Kenya |
Tarehe ya kifo | 28 Mei 2021 |
Lugha zinazozungumzwa, zilizoandikwa au zilizotiwa sahihi | Kiingereza |
Kazi | association football player |
Nafasi anayocheza kwenye timu | Beki |
Mchezo | mpira wa miguu |
Zablon Davies Amanaka (alizaliwa 1 Januari 1976) ni mwanakandanda wa kimataifa kutoka nchi ya Kenya, ambaye anaichezea klabu ya La passe FC.
Wasifu
[hariri | hariri chanzo]Baada ya kuzichezea klabu kama vile Kenya Breweries (jina la zamani la Tusker FC) na Kenya Pipeline FC kutoka Nairobi, mwaka wa 2004 aliichezea kwa muda mfupi klabu ya Ligi ya Shelisheli ya Saint-Michel United. Kutoka Januari mwaka wa 2005 hadi Januari 2006, alicheza katika Ligi Kuu ya Bosnia na Herzegovina katika klabu yenye nguvu ziadi tangu jadi nchini humo, FK Željezničar kutoka mji mkuu wa Sarajevo. Kisha alirejea kucheza katika vilabu vya Ligi ya Kenya vya Thika United na AFC Leopards. Tangu Januari hadi Juni mwaka wa 2007 alikuwa nchini Uhindi katika klabu ya I-League ya East Bengal Club. Kisha, alihamia klabu Ushelisheli ya Anse Reunion FC na tangu Januari mwaka wa 2009 alirudi katika nchi ambayo alizaliwa na sasa anaichezea klabu ya Mahakama.
Timu ya Kitaifa
[hariri | hariri chanzo]Amekuwa akiichezea timu ya kitaifa ya kandanda ya Harambee Stars mara kwa mara tangu mwaka wa 1998 na pia aliwahi kuwa nahodha wa timu ya kitaifa.[1]
Tuzo
[hariri | hariri chanzo]- Saint-Michel United
- Bingwa wa mara moja wa ligi ya Ushelisheli: 2003
- FK Željezničar
- Timu yake ilimaliza katika nafasi ya pili: 2004-05
- India East Bengal Club
- Bingwa wa mara moja wa ligi ya Uhindi: 2007
- Shelisheli Anse Reunion FC
- Bingwa wa mara moja wa kombe la ligi la Ushelisheli: 2007
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "102sports". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-08-06. Iliwekwa mnamo 2010-01-20.
Vyanzo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Article on Kangemi Utd. kuhusu Amanaka na wachezaji wengine wa Kenya Archived 18 Julai 2011 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Zablon Amanaka kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |