Nenda kwa yaliyomo

Lusiano wa Antiokia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mchoro mdogo wa kifodini chake kutoka Menologion ya Basili II.

Lusiano wa Antiokia (labda Samosata, leo Samsat, Uturuki, 240 hivi – labda Nikomedia, 7 Januari 312) alikuwa padri mwanateolojia ambaye alijulikana pia kwa uadilifu wake mkubwa na hatimaye alifia dini ya Ukristo kwa kukatwa kichwa au kwa kuachwa afe njaa[1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 7 Januari[2][1] au 15 Oktoba.

Alipata upadrisho huko Antiokia akaanzisha chuo cha teolojia ambacho kilikwenda kinyume cha chuo cha Aleksandria kwa kutaka maneno ya Biblia yasifafanuliwe kiroho mno, na badala yake yachukuliwe yalivyo.

Kwa ajili hiyo alifanya kazi kubwa ya kulinganisha nakala mbalimbali ili kuona maandiko asili yaliyopotea yalikuwaje. Eusebi wa Kaisarea alisifu utaalamu na ufasaha wake[3] na kazi hiyo ni muhimu hata leo kwa wataalamu wa Biblia. Wengine waliomsifu ni Yohane Krisostomo, Sirili wa Aleksandria na Jeromu.

Hata hivyo alihusishwa na uzushi akatengwa na Kanisa, ila baadaye alipatanishwa (285 hivi).

Chini ya kaisari Maximinus Daia, alifungwa na kupelekwa Nikomedia, alipoteswa sana akiwa gerezani miaka tisa bila kukubali kuasi dini yake. Hatimaye aliuawa.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. 1.0 1.1 Attwater, Donald and Catherine Rachel John. The Penguin Dictionary of Saints. 3rd edition. New York: Penguin Books, 1993. ISBN|0-14-051312-4.
  2. Martyrologium Romanum
  3. Church History IX, 6, 3.
  • Gustave Bardy. Recherches sur saint Lucien d'Antioche et son école (Paris: Beauchesne, 1936).
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.