Nenda kwa yaliyomo

Kupatwa kwa Jua

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Kupatwa kwa jua)
Kupatwa kwa Jua tar. 29 Machi 2006

Kupita kwa kivuli cha mwezi duniani wakati wa kupatwa kwa Jua. Watu katika eneo kubwa la giza waliona kupatwa kwa Jua kisehemu. Nukta nyeusi yaonyesha sehemu ya "umbra" ambako Jua lilipatwa kabisa. Duara kubwa zaidi ya kijivu linaonyesha maeneo katika "penumbra", yaani kivuli cha kando.
"Central duration" inataja muda wa kupatwa kabisa kwenye kitovu cha kivuli; namba katika kona ya juu huonyesha saa za tarehe 29 Machi kupatwa kulipotokea.

Kupatwa kwa Jua (kwa Kiingereza solar eclipse) ni hali ya Jua kutoonekana (au kuonekana kwa sehemu tu) angani wakati wa mchana kwa muda fulani hata pasipo mawingu. Kunatokea wakati mwezi unapita kati ya Jua na dunia na kufunika Jua. Tokeo lake ni kupungua kwa nuru ya Jua hadi kutoonekana kwa muda wa kufika kwa giza wakati wa mchana. Muda wa kufunikwa kabisa ni dakika chache tu.

Kuna utofauti kati ya “Kupatwa kiasi” (ing. partial eclipse) na “Kupatwa kikamilifu” (ing. total eclipse). Kupatwa kwa Jua hutokea kila mwaka, angalau mara mbili hadi mara tano. Lakini kupatwa kabisa kwa Jua hautokei zaidi kuliko mara mbili kwa mwaka.[1][2]. Huonekana katika sehemu za Dunia pekee, si kote.

Misingi ya kupatwa kwa Jua

Kupatwa kwa Jua kunatokea wakati Mwezi unapita kati ya Jua na Dunia. Hapo Jua, Mwezi na Dunia zinakaa kwenye mstari mmoja mnyoofu. Katika hali hiyo Mwezi hurusha kivuli chake kwenye uso wa Dunia. Kivuli hiki hakifuniki Dunia yote. Ni kama kinu kwenye uso wa Dunia. Nje ya kivuli hiki Jua linaonekana kwa sehemu au bila upungufu.

Hali ya kupatwa kabisa kwa Jua inatazamwa kila mara kwenye mstari mwembamba kwenye uso wa Dunia, tena giza kabisa kwa muda mfupi. Mstari huu ni njia ya umbra au kitovu cha kivuli chake kwenye uso wa Dunia. Nje ya njia hii kupatwa kwa Jua kunaonekana kisehemu tu katika sehemu zinazoathiriwa na penumbra au kivuli cha kando cha Mwezi. Mbali na njia ya kivuli hiki Jua linaonekana kama kawaida.

Aina za kupatwa kwa Jua

Kuna aina mbalimbali za kupatwa kwa Jua.

  • kupatwa kikamilifu: Jua hupotea kabisa kwa dakika chache. Hali hii yaonekana kwenye ukanda mwembamba duniani pale ambako kitovu cha kivuli kinapita.
  • kupatwa kipete: mwezi huonekana mdogo kiasi kuliko Jua. Kwa hiyo duara la mwangaza wa Jua ni kubwa kuliko duara la Mwezi na mwanga wa Jua huonekana kama pete.
  • kupatwa kwa Jua kiasi: Katika eneo kubwa la kivuli cha kando watu huona upungufu wa mwanga; kiasi chake hutegemea umbali wa kitovu cha kivuli. Wakitazama Jua kwa kichujio, kwa mfano kioo kilichopakwa dohani kutoka moshi wa mshumaa, huwa wanaona sehemu ya duara ya Jua imefunikwa.

Mpito wa sayari

angalia Mpito wa Zuhura Wakati sayari inapita kati ya Jua na Dunia inafunika sehemu ya Jua. Tofauti haionekani kwa macho lakini inaweza kutazamwa kwa kutumia darubini. Kuna sayari mbili zinazoweza kupita mbele ya Jua kwa macho ya mtazamaji duniani, ni Utaridi (Mercury) na Zuhura (Venus).

Tazama pia

Marejeo

  1. Littmann, Mark (2008). Totality: Eclipses of the Sun. Oxford University Press. ku. 18–19. ISBN 0199532095. {{cite book}}: Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help)
  2. Kupatwa kwa Jua kulitokea mara tano katika mwaka 1935 NASA (6 September, 2009). "Five Millennium Catalog of Solar Eclipses". NASA Eclipse Web Site. Fred Espenak, Project and Website Manager. {{cite book}}: |access-date= requires |url= (help); Check date values in: |date= (help); External link in |chapterurl= na |title= (help); Unknown parameter |chapterurl= ignored (|chapter-url= suggested) (help)

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Usalama wa macho wakati wa kuangalia

Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kupatwa kwa Jua kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.