Nenda kwa yaliyomo

Kiboko Kibete

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Kiboko kibete)
Kiboko kibete
Kiboko kibete kwenye Bustani ya Wanyama ya Rostock
Kiboko kibete kwenye Bustani ya Wanyama ya Rostock
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele)
Nusungeli: Placentalia (Wanyama wenye mji)
Oda: Artiodactyla (Wanyama wenye kwato mbili kwa kila mguu)
Nusuoda: Whippomorpha (Wanyama kama nyangumi na viboko)
Familia: Hippopotamidae (Wanyama walio na mnasaba na kiboko)
Jenasi: Choeropsis
Leidy, 1853
Spishi: C. liberiensis
(Morton, 1849)
Ngazi za chini

Nususpishi 2:

Kiboko kibete (Choeropsis liberiensis) ni kiboko mdogo wa familia Hippopotamidae, ambaye asili yake ni misitu na vinamasi vya Afrika ya Magharibi, hasa Liberia pamoja na idadi ndogo nchini Sierra Leone, Gini na Kodivaa. Ameangamizwa huko Nijeria[1]. Anafanana na binamu yake mkubwa, kiboko wa kawaida.

Kiboko kibete hujitenga na kukiakia usiku. Anaonyesha matohozi mengi ya nchi kavu, lakini kama kiboko wa kawaida huishi majini na kutegemea maji ili kuweka ngozi yake unyevu na halijoto ya mwili wake kuwa wastani. Mienendo kama vile kupandana na kuzaa inaweza kutokea majini au nchi kavu. Kiboko kibete ni mlamani na hula kangaga, mimea yenye majani mapana, nyasi na matunda anayopata msituni. Kwa kuwa hukiakia msituni usiku na ni adimu, kiumbe huyu ni mnyama mgumu kuchunguza porini.

Viboko vibete hawakujulikani nje ya Afrika ya Magharibi hadi karne ya 19. Waliwasilishwa kwenye bustani za wanyama mwanzoni mwa karne ya 20 na walijitokeza kuzaliana vizuri ufungwani. Kwa hivyo uchunguzi mwingi sana umepatwa kutoka wanyama kwenye bustani[2]. Kuokoa kwa spishi hii ufungwani ni kwa uhakika zaidi kuliko porini. Mwaka 2015 ukadirifu wa IUCN umeonyesha kwamba idadu ya viboko vibete wanaobaki porini ni chini ya 2500[1].

Viboko vibete kimsingi wanatishiwa na kupotea kwa makazi, kwani misitu hukatwa na kugeuzwa kuwa maeneo ya shamba, na pia wako katika hatari ya ujangili, kuwinda nyama ya msituni, mbuai wa kiasilia na vita. Viboko vibete ni miongoni mwa spishi zinazowindwa kinyume cha sheria kwa ajili ya chakula nchini Libeŕia.

  1. 1.0 1.1 Ransom, C.; Robinson, P.T.; Collen, B. (2015). Choeropsis liberiensis. IUCN Red List of Threatened Species.
  2. Stroman, H. R.; Slaughter, L. M. (Januari 1972). "The care and breeding of the Pygmy hippopotamus (Choeropsis liberiensis) in captivity". International Zoo Yearbook. 12 (1): 126–131. doi:10.1111/j.1748-1090.1972.tb02296.x.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)